Ukikaa Kijiji Beach ama Chadibwa Beach kuanzia muda wa asubuhi mpaka mchana milio ya mshindo kutoka baharini ni kitu cha kawaida kwa mara ya kwanza utashtuka baadaye utazoea kwani hawa jamaa wanafanya bila kuogopa na ni mfululizo, Kwa wakazi wa Kigamboni jambo hili kwa sasa limekuwa kawaida kwani ukitembelea fukwe za kuanzia Chadibwa Beach na Kijiji Beach ambayo ni Kilometa 3 tuu kutoka Kigamboni Ferry hadi South Beach ambayo ni takribani 7 Kilometa kila baada ya nusu saa hadi dakika 45 utasikia mlio mshindo ukitokea maeneo ya baharini na kama macho yako yakiwahi utaona maji yakiruka juu kama picha inavyoonyesha, si kingine ni wavuvi wa kutumia baruti.
Kinachosikitisha zaidi hawa jamaa hawaogopi kupiga baruti zao, ikumbukwe kuwa ni takribani nusu kilomita kutoka Kambi ya jeshi ambayo iko pembezoni mwa Mikadi Beach. na si mbali kutoka ufukweni wanakuwa mahali ambapo hata ukimuita mtu anakusikia.
Tumeambiwa kuwa uvuvi huu mbali tuu kuua samaki na mazalia yao pia unaua viumbe vingine vya baharini.
Polisi wanawajua na taarifa wanazo kwani hata wakipigiwa simu wanaishia kusema tunakuja na hakuna kinachotokea, Mmiliki wa Kijiji Beach alijitahidi sana kutoa taarifa bila mafanikio na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa mpaka sasa amekata tamaa. Inakera sana, tunaomba wahusika walivalie njuga na kulifanyia kazi suala hili.
Mdau Pius.



Kwa hili tukisema polisi wanahusika watajibu nini? jamani watazania mbona tunavichwa vya nazi? Nchi yetu ina neema ya kila aina lakini inasikitisha umaskini tulionao sio tu wa fedha lakini wa elimu na hekima hatuna si msomi wala kabwela wote sawa... hivi hili la baruti inakuwaje jamani? sasa watataka kuunda tume ya uchunguzi wale fedha za vikao tena na magari ya kifahari waende kigamboni na beach au labda boti la kifahari lenye air condition wazunguke baharini...
ReplyDeleteHongra mtoa taarifa kwa kupata hadi picha..... we kweli mzalendo angalia usije kulipuliwa wewe....
Kiukweli suala hili linakera sana, na imekuwa kama jambo la kawaida kwa wakazi wa Kigamboni kutumia samaki hao wanaovuliwa kwa uvuvi wa kutumia baruti, niliwahi kusoma kwenye makala moja katika mitandao hii ya kijamii ila sina kumbukumbu nzuri ulikuwa ni mtandao gani! Iliripotiwa kuwa utumiaji wa samaki wanaovuliwa kwa baruti au mabomu unaweza kusababisha athari za kansa kwa mtumiaji! Ni hatari sana, na nadhani mamlaka husika watalifanyia kazi suala hili haraka iwezekanavyo, wakishindwa watupe mamlaka wananchi tujichukulie sheria mkononi!
ReplyDeletepole sana mdau,kwa kweli mimi nashangaa polisi wa kitanzania huwa wanavalia njuga kitu cha kawaida,ila kitu cha hatari kama hicho huwa wanapuuza,sasa sijui kuna nini ndani yake,,Hiki kitu kinasikitisha mno mno.
ReplyDeleteAnkal tunakuomba maswala kama haya,utusaidie utufikishie kilio hiki kwa wahusika wakuu,ili wavuvi hao wafikishwe katika vyombo vya sheria,ili uwe mfano kwa wengine na uvuvi haramu usiendelee.
Ahlam,,UK
Basi ukiona polisi hawashiriki jambo ujue liwahusu,jaribu kuchunguza kwa makini utaligundua hilo,fanya urafiki nahao jamaa,utapata kujua kwa ukamilifu nimradi wa nani,maana wizara husika imekataza katakata uvuaji huo,je jeshi la polisi ambalo ndio linatakiwa kutii sheria linavunja,hapo kuna jambo.
ReplyDeleteAsalaam Alaikum, bw Michuzi hizi ndio habari za msingi kuweka hawa wavuvi na Askari lao moja. MZ
ReplyDeletemI SIELEWI KWANINI MAMALAKA HUSIKA WANAZIBA MACHO NA WANAFUNGA MASIKIO KUCHUKUA HATUA...HATA UFUKWE WA COCO BEACH WANALIPUA ILE MBAYA
ReplyDeleteHiyo ni miradi ya wazee , wala usiseme kitu. vingozi wa nchi hii wako juu ya sheria
ReplyDeletekaka ndugulile kazi yako hiyo nafikiri utasoma ama utaambiwa!Nahisi polis kigamboni niwazembe sana na sijui kwanini nyinyi viongozi hamuwasafishi iko wazi kabisa maana mpaka mimi raia wakawaida kuona kama polisi niwazembe kigamboni inamaana hakuna chakuficha!
ReplyDeleteAnkal Michuzi,
ReplyDeleteNashukuru kwa kutuma hii posting hapa. hili suala ni la kawaida sana hasa katika maeneo uliyoyataja, na hakuna kuogopa wala kuchukuliwa hatua wanafanya wazi wazi tu.
Jambo lingine ni kuwa Serikali ilisimamisha shughuli za ujenzi na kuendelea maeneo kwa ajili mji mpya Kigamboni. Lakini sasa Wadau wamegeuza Kigamboni machimbo ya kokoto na kifusi, hili linafanyikja wazi wazi hata usoni mwa South Beach Residential maeneo ambayo Manispaa ya Temeke ingekuwa inayategemea na kujivunia. Hili lisipochukuliwa hatua na Uvuvi haramu wa baruti Kigamboni itageuka kuwa kama Kunduchi.
Wenyewe wapo wanaangaliua kwingine.
Mdau.
tunangoja wamarekani watoe msaada kuzuia uvuvi haramu ndio tuanzishe kitengo maalum,chenye boss mwenye V8 na maafisa wengine 30,waende kozi miezi mitatu kisha tufanye semina elekezi kwa maafisa wetu na katikati ya mwaka 2014 ndio tutaunda tume kushughulikia hilo,usijali mkazi wa kigamboni,ufukwe wa coco na wewe unaepita na boti za kwenda zenji,kwani ikitokea ajali meli kulipukiwa na bomu itakuwa ni fursa ya kuitangaza nchi katika vyombo vya habari vya kimataifa kama Al Jazeera,CCTV, RT, BBC na wanazalendo CNN.
ReplyDeleteHili jambo limekuwa linaeandelea kwa MIAKA!!! haraka haraka SIO CHINI YA MIAKA 25 maana miaka 25 iliyopita kuna jamaa alikatika mkono pale feri kuanzia kwapani, wakawa wanamuita CARWASH! sijui kama bado yupo hai.
ReplyDeleteInasikitisha SANA, poiosi wanaona, wanajeshi wanaona, maafisa wa ikulu wanaona lakini HAKUNA CHOCHOTE kinachofanyika.
Matokeo yake mazalio ya samaki na viumbe vingine baharini yanazidi kuharibika.
Tumekalia maneno tuuuuuuuu!!!!
Kama n Polisi wenyewe wa Kigamboni na Mjimwema tusahau kabisa ,Polisi wa vituo hivyo ni wazembe sana,nakumbukuama lile tukio la mwaka jana mwezi 8,wanajeshi wa JWTZ walivyovamia makazi na mashamba ya raia wa kijiji cha Kimbiji,Polisi walikataa kabisa kupokea taarifa,na mkuu wa Polisi wa mkoa Temeke ,RPC Misime huyu ndio sahau kabisa kabisa
ReplyDeleteHuu ni Msala unaowahusu Askari Jeshi Wapinaji Kikosi cha Maji JWTZ-NAVY tena imekaa vizuri wapo huko huko Kigamboni!
ReplyDeleteHawa Navy wanazo Speed Tags, yaani Boti ziendazo kasi!
Sasa kama ni Ulinzi na uhalifu wenyewe unahusisha dalili kuu hizi:
1-Milipuko ya Baruti,(moto)
2-Ni wapi wanapata Baruti,
3-Milipuko inatoa taharuki kwa watu,
4-Hata mvuvi mwenyewe akikaa vibaya bila tahadhari wakati wa mlipuko anaweza pata madhara lich ya wengine,
Walaumiwe nani kama sio Navy ya Jeshi?
Polisi wa Bongo wapo ki Saccos zaidi kuliko kiutendaji!
ReplyDeleteWao wapo makini ktk masuala na mikasa inayo ashiria 'mkono kwenda kinywani' tu!
Lakini kwenye mambo kama haya ya mabaruti kulipuka na misuko suko Lohhh Polisi wa Bongo ndipo utakapo staajabu maajabu ya Mussa...Polisi ile anasikia mlipuko anakimbia akiona spidi yake ndogo mabuti mazito miguuni anayavua na anakula kona!
Kwani masihara?
Tuliwashuhudia siku ya Mabomu kulipuka Mbagala Polisi sambamba na raia walikimbia !
Polisi wanaangalia mshiko zaidi, hiyo mibomu ohhh utawatafuta !
ReplyDeleteKulipukiwa na mibaruti?
ReplyDeleteAskari wa Kibongo wapo kama 'Chuma ulete' wao wanashughulikia gemu zinazozaa 'ngawira' wapo ki pesa zaidi!!!
Polisi wa Kibongo wao ni rushwa pekee,kwanza hiyo mibomu wanatoka nduki wanakaa mbali baada ya tukio ndio wanakuja!
ReplyDelete