Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akiongea jambo kwenye mjadala wa NGOs round table uliofanyika Alhamisi May 31, 2012, Washington, DC.
Mhe. kaimu Balozi Lilian Munanka akisisitiza jambo, Mhe. Munanka ndie aliyeongoza mjadala wa NGOs Round Table uliofanyikia Washington, DC
Bw. Ikomba E. Mathew ambae ni Afisa wa Uhamiaji upande vibali vya kufanyia kazi akielezea utaratibu unaotakiwa kufuata unapokua unaomba kibali cha kufanyia kazi Nchini Tanzania.
Trina Gunn Afisa wa Peace Corps akielezea jambo katika muendelezo wa mjadala wa NGOs round table uliofanyika Alhamisi May 31, 2012, Jijini Washington, DC.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akielezea taratibu za chanjo unapokua unasafari ya kwenda Tanzania.
Kelly Daly ambae ni Officer for Tanzania U.S. Agency For International Deleopment (USAD) ambae ameishafanya kazi Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania akielezea utaratibu wa nini cha kufanya kwa Wamarekani waotembelea Tanzania.
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akimsikiliza mmoja ya mwanaNGOs aliyekua anataka ufafanuzi wa jambo fulani, kati ni Afisa Ubalozi Dr. Mkama.


Ankal kunani huko Washington na balozi Maajar? Mbona kila kukicha ni habari za huyu mama na wadau wa Washingtong, in maana hakuna balozi nyingine za Tz huko abroad zinazoendesha shughuli za maendeleo? Give us a little break ankal!
ReplyDeleteAsanteni kwa taarifa. Nilikua natoa angalizo la matumizi ya Lugha. Mara nyingi nimekua nikiona Ms Lilian Munanka akitabulishwa kama "kaimu balozi" siku zote nikiona hivyo huwa nachukulia kwamba balozi hayupo an bi Munanka anakaimu (acting) nafasi ya balozi. Lakini katika tukio hili wote wawili wapo na bado anatambulishwa kama 'kaimu balozi". Nadhani mlikuwa na nia ya kumtabulisha kama 'deputy' na kama ni hivyo, neno sahihi ni 'naibu balozi'
ReplyDeletekaka Michuzi,
ReplyDeletenaomba usahihishe, huyu Lilian Munanka ni ofisa wa ubalozi tu mwenye cheo cha mkuu wa utawala/Mkurugenzi Msaidizi. Hana hadhi yeyote ya 'uheshimiwa" wala "ukaimu Balozi". Atakaimu vipi wakati balozi husika yuko kituoni. mtumishi pekee mwenye hadi ya Ubalozi hapo kituoni Washington DC ni Mhe. balozi Mwanaidi Maajar. Wengine kama wanaojiita mabalozi, au makaimu wamejipachika tu.
haya makosa yamekuwa yakijirudia sana na ni ukiukwaji wa hali ya juu wa taratibu za kidiplomasia.
Mdau,
Chuo cha Diplomasia-DAR
Annon.1 Mon. 4/6 03:17, ukiona hivyo ujue kwamba hakuna Balozi zingine zinazoendesha shughuli za maendeleo,la sivyo nazo ungeziona kwenye mtandao. Mpeni haki yake huyu mama kwa kazi nzuri anayoifanya.
ReplyDeleteWengi wetu (na mimi nikiwa mmoja wao)tunasumbuka sana katika utumiaji sahihi wa KAIMU/NAIBU/MSAIDIZI...nk. Inapendeza sana kuwasikiliza wataalamu kama hawa waliotangulia wanaojaribu kutusahihisha.
ReplyDeleteUsahihi zaidi. Wall siyo deputy. L'abda Mseme amesahaulika katika mchakato wa juzi. Yeye ni assistant director/minister plen.../afisa ubalozi. ......of corse ni senior officer sana tu ila hajaqualify Kwenye Huo ubalozi ambao yeye/wanaglob/wananchi/ wanauota......
ReplyDeleteBalozi maajar amechangamka. Mabalozi wengine hata hatuwajui majina Yao. Wamelala usingizi. Mama chapa kazi ila usilete siasa za kwa malkia.
ReplyDeleteJamani mama Maajar anafanya kazi yake apongezwe na apewe ushirikiano!
ReplyDeleteNchi zingine Mabalozi wanawakimbia Wananchi wa Tanzania kwa kuogopa kusahihishwa, kukwepa majukumu na kutolewa matatizo!!!
Assalama Lakko zake Balozi Mwanaidi S. Maajar!!!
ReplyDeleteHuyu mama anafanya kazi pevu kabisa tofauti na Mabalozi wetu nchi zingine ukimjumuisha Mhe. Peter Kallaghe wa Uingereza pia ni mfano wa kuigwa !