Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akiongea jambo kwenye mjadala wa NGOs round table uliofanyika Alhamisi May 31, 2012, Washington, DC.
Mhe. kaimu Balozi Lilian Munanka akisisitiza jambo, Mhe. Munanka ndie aliyeongoza mjadala wa NGOs Round Table uliofanyikia Washington, DC
Bw. Ikomba E. Mathew ambae ni Afisa wa Uhamiaji upande vibali vya kufanyia kazi akielezea utaratibu unaotakiwa kufuata unapokua unaomba kibali cha kufanyia kazi Nchini Tanzania.
Trina Gunn Afisa wa Peace Corps akielezea jambo katika muendelezo wa mjadala wa NGOs round table uliofanyika Alhamisi May 31, 2012, Jijini Washington, DC.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akielezea taratibu za chanjo unapokua unasafari ya kwenda Tanzania.
Kelly Daly  ambae ni Officer for Tanzania U.S. Agency For International Deleopment (USAD) ambae ameishafanya kazi Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania akielezea utaratibu wa nini cha kufanya kwa Wamarekani waotembelea Tanzania.
 
Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akimsikiliza mmoja ya mwanaNGOs aliyekua anataka ufafanuzi wa jambo fulani, kati ni Afisa Ubalozi Dr. Mkama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2012

    Ankal kunani huko Washington na balozi Maajar? Mbona kila kukicha ni habari za huyu mama na wadau wa Washingtong, in maana hakuna balozi nyingine za Tz huko abroad zinazoendesha shughuli za maendeleo? Give us a little break ankal!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2012

    Asanteni kwa taarifa. Nilikua natoa angalizo la matumizi ya Lugha. Mara nyingi nimekua nikiona Ms Lilian Munanka akitabulishwa kama "kaimu balozi" siku zote nikiona hivyo huwa nachukulia kwamba balozi hayupo an bi Munanka anakaimu (acting) nafasi ya balozi. Lakini katika tukio hili wote wawili wapo na bado anatambulishwa kama 'kaimu balozi". Nadhani mlikuwa na nia ya kumtabulisha kama 'deputy' na kama ni hivyo, neno sahihi ni 'naibu balozi'

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2012

    kaka Michuzi,
    naomba usahihishe, huyu Lilian Munanka ni ofisa wa ubalozi tu mwenye cheo cha mkuu wa utawala/Mkurugenzi Msaidizi. Hana hadhi yeyote ya 'uheshimiwa" wala "ukaimu Balozi". Atakaimu vipi wakati balozi husika yuko kituoni. mtumishi pekee mwenye hadi ya Ubalozi hapo kituoni Washington DC ni Mhe. balozi Mwanaidi Maajar. Wengine kama wanaojiita mabalozi, au makaimu wamejipachika tu.
    haya makosa yamekuwa yakijirudia sana na ni ukiukwaji wa hali ya juu wa taratibu za kidiplomasia.

    Mdau,
    Chuo cha Diplomasia-DAR

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    Annon.1 Mon. 4/6 03:17, ukiona hivyo ujue kwamba hakuna Balozi zingine zinazoendesha shughuli za maendeleo,la sivyo nazo ungeziona kwenye mtandao. Mpeni haki yake huyu mama kwa kazi nzuri anayoifanya.

    ReplyDelete
  5. Wengi wetu (na mimi nikiwa mmoja wao)tunasumbuka sana katika utumiaji sahihi wa KAIMU/NAIBU/MSAIDIZI...nk. Inapendeza sana kuwasikiliza wataalamu kama hawa waliotangulia wanaojaribu kutusahihisha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2012

    Usahihi zaidi. Wall siyo deputy. L'abda Mseme amesahaulika katika mchakato wa juzi. Yeye ni assistant director/minister plen.../afisa ubalozi. ......of corse ni senior officer sana tu ila hajaqualify Kwenye Huo ubalozi ambao yeye/wanaglob/wananchi/ wanauota......

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2012

    Balozi maajar amechangamka. Mabalozi wengine hata hatuwajui majina Yao. Wamelala usingizi. Mama chapa kazi ila usilete siasa za kwa malkia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2012

    Jamani mama Maajar anafanya kazi yake apongezwe na apewe ushirikiano!

    Nchi zingine Mabalozi wanawakimbia Wananchi wa Tanzania kwa kuogopa kusahihishwa, kukwepa majukumu na kutolewa matatizo!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2012

    Assalama Lakko zake Balozi Mwanaidi S. Maajar!!!

    Huyu mama anafanya kazi pevu kabisa tofauti na Mabalozi wetu nchi zingine ukimjumuisha Mhe. Peter Kallaghe wa Uingereza pia ni mfano wa kuigwa !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...