Msafiri Zawose mtoto wa marehemu Hukwe Zawose akiwa kwenye darasa lake la kufundisha ngoma za asili kutoka Tanzania picha ni Msafiri Zawose akiwa Bloombars Dance Studio iliyopo, Washington, DC, NW, yeye hua anasafiri Nchi mbalimbali kufundisha uchezaji wa ngoma za asili kutoka Tanzania hasa kutoka kwenye kabila lake la Wagogo.
 Masafiri Zawaose akiwa darasani akifundisha huku akisaidiwa na mke wake Hanah Zawose (kulia) kati ni mmoja ya wanafunzi wake, Winter Allen.
 Juu na chini ni Msafiri Zawuse akiendelea na darasa lake la kufundisha ngoma za asili jijini Washington, DC, NW
 Msafiri Zawose akiwa na mkewe, Hanah Zawose wakipata picha ya pamoja
Msafiri Zawose (wapili toka kushoto) akiwa na wanafunzi wake kutoka kushoto ni John Chumbers, yeye, Winter Allen na Mke wake Hanah.

Msafiri anapatikana kwa shughuli za aina zote kama vile Harusi na shughuli maalum yeye ni mtaalam wa ngoma za asili atakuwepo Marekani Mpaka Aug 8, 2012 kampuni yake inaitwa ART PROMOTERS FOUNDATION na unaweza mtembelea msafirizawose.wordpress.com/art-promoters/ na pia unaweza wasiliana nae kupitia-simu:             +255 784 829 218       au             865 591 5257      
                        barua pepe: mzawose@gmail.com
                        Store: esty.com/shop/mzawose
                        Music:msafirizawose.bandcamp.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2012

    Huyu ana bahati amepata blonde, sio bure.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2012

    sio bure labda aliaga kwao

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2012

    sio blonde, ni brunette or red hair.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2012

    Na wewe nenda kwenu kaage uone kama utabarikiwa kubwa jinga!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2012

    We mtoa maoni wa kwanza unatuaibisha kweli sisi waafrika na ulimbukeni wako: eti "ana bahati amepata blonde." Angekuwa mdengereko kwani shida iko wapi? kwani blonde ndiyo bora zaidi? Mshamba bwana utamjua tu. We ungesema, ana bahati kapata mke mzuri ingetosha tu. Sasa ukianza kugusia rangi yake ndiyo unaharibu. Jipende mwafrika, ngozi ya chocolate imeumbika bwana, hata muumba mwenyewe kaikubali. Elimika kijana na ijue historia yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...