NYUMBA INAUZWA NJIRO KWA MSOLWA , ARUSHA MITA 10 TOKA BARABARA KUU YA KWENDA THEMI ESTATE.Nyumba ni ya ghorofa,JUU kuna master bedroom yenye kabati kubwa la nguo,water heater,spilit unit,taa za kisasa,changing room,bath cube,bath tab,hand wash basin,bidets,toilet varanda kubwa mbili yenye view ya mlima kilimanjaro,na mlima meru,vyumba viwili vya kulala self contain na varanda kubwa heater ya maji,study room kubwa,mini sitting room.

CHINI kuna guest room self contain yenye kabati la nguo,bath cube,heater,hand wash basin.Dinning ina hand wash basin,taa za kiasasa,sitting room taa za shandria,spirit unit ndefu,door camera,public toilet,laundry,stoo,jiko kubwa lenye kitchen cabnet, jiko la gesi,drier ya vyombo.

Nyumba ina tiles nyumba nzima,vioo vya aluminium,vigae vya Nabaki Africa,gata za kuvuna maji,reserve tank,taa za garden na security,geti la kuslide,nyumba mpya kabisa ina umeme wa tanesco na maji ya dawasco.muuzaji ni mwenye nyumba,dalali hatakiwi.Kwa mawasiliano piga simu             +255756666708, email mwijo70jojo@yahoo.co.uk Kazi njema  .Picha zadi Bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2012

    Ok tumekupata ila nadhani inatakiwa isomeke "split unit" badala ya "spirit unit". Tunalifikiria. Ichube

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2012

    Muuzaji tutajie basi angalau bei ya kuanzia hapa kabla hatujaanza kukupigia simu?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2012

    maji ya DAWASCO? ARUSHA?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2012

    Maji ya DAWASCO? ARUSHA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2012

    ..dah, hivi Arusha kuna maji ya DAWASCO!!! tehe tehe teh!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2012

    ANONY. NO 1 - WATU WAKO KWENYE BIASHARA, WEWE UNASAHIHISHA SPELLING SII INAELEWEKA HATA HIVYO.NYUMBA NI NZURI SANA WENYE HELA ZAO RUKSA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2012

    ichube wewe kama mnunuzi kweli ya nini kujifanya mjuaji wa lugha za wenzako makosa madogo madogo eti kujidai kukosea mkuu vipi wewe ukitaka nunua nyumba au kodi wacha zako hizo

    please jambo mmoja naomba mwenye nyumba weka contact zako ili nikitaka kuwasiliana na wewe nikupate vipi mkuu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 12, 2012

    sasa mjamaa weka bei basi , mimi nitoke huku dar mpaka Arusha kwa kukifuata kitu hata bei siijui.

    nyumba nzuri ndio nimeipenda, lakini kama ni ya kuuzwa au kukodishwa lazima bei iwe inajulikana au iweke kwenye site au kurasa za mauzaji ya n yumba ili bei iwe wazi

    ReplyDelete
  9. Kaka TrioJune 12, 2012

    Unauza au kupangisha nyumba halafu bei hutundiki manake nini?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 12, 2012

    Ili kupunguza usumbufu wa kupigiwa simu (Wabongo nadhani unawajua), waonaje uweke bei kabisa!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 13, 2012

    MIJITU HAINA HATA ELFU KUMI MFUKONI AFU INAJITIA KUSAHISHA SPELL MISTAKE...U MUCH KNOW TU UMEWAJAA, NDO MAANA MNAKUFA MASKINI, KWA SABABU YA MAJUNGU NA UJUAJI MWINGI

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2012

    Mamlaka ya maji Arusha inaitwa AUWASSA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2012

    Msijihangaishe asking Price is TSH. 500 Million!

    Asiyekuwa na hela inayokaribia hapo wala hata kusahihisha spelling asifanye aendelee na mengine!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 13, 2012

    HIVI NYUMBA ULIJENGA ILI UUZE AU UKAE MWENYEWE, KWANI KUNUNUA NYUMBA KAMA HII HATUI FOUNDATION IKO JE, MATANKI YA MAJI MACHAFU HAYARUDISHI MAJI NDANI N.K. NYIE MNATAKA KUNUNUA MUWE WAANGALIFU SANA.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 13, 2012

    Mwenye kuwa na vitu vikubwa vitatu :

    1.PESA kuanzia TSHS. 10 Million angalau.
    2.BIASHARA HALALI inayo fanyika na mzunguko mzuri.
    3.AWE MTEJA WA BENKI MAKINI.

    Mtu wa aina hiyo ndiyo ajitahidi kuuliza ni vile hata kama atakuwa chini ya bei anaweza kuongea na Benki yake akalipiwa kununua na Benki halafu yeye akarejesha taratibu deni Benki (WANAITA MORTGAGE AND RE-FINANCING FACILITY)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...