
Kalamu ninaishika, kwa majonzi na huzuni,
Machache kuyaandika, kihoro kiko moyoni,
Gwiji kweli katutoka, tulimpenda kifani,
Profesa Mutakyahwa, ulale mahali pema.
Prof. alibobea, katika miamba moto,
Tabaka na Geu pia, mambo ya kimchakato,
Mazingira kukazia, alitoa changamoto,
Profesa Mutakyahwa, ulale mahali pema.
Mahiri katika fani, mcheshi na wa mfano,
Miamba kafundisheni, tafiti zenye muono,
Faida hapa nchini, wengi waunga mkono,
Profesa Mutakyahwa, ulale mahali pema.
Wajiolojia nchini, tumepoteza kipenzi,
Mawazo yalo makini, inabidi tuyaenzi,
Idara ‘’Jiolojia’’, Mlimani kwa ‘’pamoja’’,
Prof. nenda salama, daima tutakumbuka.
Mola awape baraka, walofikwa na msiba-a
Familia kwa hakika, Rabuka atajalia,


R.I.P Prof."Mutta" kipindi ukiwa bado Doctor,natakukumbuka sana kwa ukarimu wako na ufundishaji wako.Binafsi nakukumbuka sana kwenye somo la Industrial minerals in Tanzania,ukatupeleka hadi Pugu Kaolin kutuonyesha kiwanda cha Kaolin kilivyokufa na kuchakaa wakati pale kuna 'reserve' ya kutosha ya Kaolin,matokeo yake Tanzania inaagiza chupa za bia,soda,kioo,nk kutoka nje!!Nitakukumbuka sana kwny somo la Sedimentology.R.I.P
ReplyDeleteHii ni nzuri sana! Watu wote tuliopitia mikononi mwa Prof. Mutakyahwa tumebaki wakiwa na hatuna uhakika kama hii pengo alilotuachia litazibika! Alikuwa mwalim, rafiki, mzazi, mlezi na zaidi ya yote hazina yetu ya ushauri...sasa tutakimbilia wapi tukiitaji ushauri wako? Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Prof. Mutakyhwa!
ReplyDeleteAnkal vipi? Hili shwairi hujalimalizia kabisa. Mbona misitari miwili tu katika ubeti wa mwisho!!! Hata Mwandishi hayupo au ndo mambo vodafasta. Kaka Michuzi, litendee haki basi hili shairi.
ReplyDeleteBuriani Profesa wa Miamba, umeacha mambo ya muhimu sana hasa katika kunoa vijana katika mambo ya miamba.