Wachezaji wa timu ya Soka ya Taifa ‘Kilimanjaro Taifa Stars’ wakijifua kwenye Uwanja wa kituo cha Michezo mjini Abidjan kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika kesho kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.
Kocha wa timu ya Soka ya Taifa ya ‘Kilimanjaro Taifa Stars’, Kim Poulsen akiwapa mazoezi ya viungo wachezaji wa timu hiyo kwenye uwanja wa kituo cha Michezo mjini Abidjan kujiandaa na michuano ya mchujo wa kucheza kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.
Asante blog ya jamii kwa updates.Mimi ndiyo wale wenye roho ya paka.Mimi siamini kama Ivory coast watatufunga 6-0.Kandanda ni mchezo wa maajabu!Vijana chezeni mpira,msiogope majina.Ni bidii tu na kujituma,fuateni maelezo ya kocha.Wapinzani wetu wataingia kwa kutudharau.Uwanja siyo mgeni kwa bahadhi ya wachezaji.Kila la Kheri
ReplyDeleteDavid V
Hawa wachezaji wetu hivi unavyowaona tu basi wao wenyewe washajuwa kuwa washafungwa tayari
ReplyDeletehawa nikuwapeleka airport wakarudi tu tena ila hapa hamna shauri
Tatizo wa TZ hatuna shukurani. Timu ikishinda ooh imebahatisha, ikifungwa ooh tulisema hakuna timu hapo, ikitoa sare ooh timu pinzani iltudharau ngoja mechi ijayo. Nacho ona watu wachache wapiga domo tena wasiyo itakia mema nchi ndiyo wako hiki.KUWENI WAZALENDO NA NCHI YENU.KAMA HAMUWEZI UZALENDO HAMIENI HUKO KWA WANAOJUA KUCHEZA MPIRA,tuacheni sis Wa TZ original.
ReplyDeleteHapa ni kichapo cha mbwa mwizi, mpira hauchezi kwa ulimi, kama ingekua tunashindana kuongea tungeshinda vizuri sana.
ReplyDeleteIvory Cost watafungwa!
ReplyDeleteIvory Coast 4 vs Tanzania 0
ReplyDeleteKAZENI BUTI MPIRA DAKIKA TISINI
ReplyDelete