Wachezaji wa timu ya Soka ya Taifa ‘Kilimanjaro Taifa Stars’ wakijifua kwenye Uwanja wa kituo cha Michezo mjini Abidjan kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika kesho kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.
Kocha wa timu ya Soka ya Taifa ya ‘Kilimanjaro Taifa Stars’, Kim Poulsen akiwapa mazoezi ya viungo wachezaji wa timu hiyo kwenye uwanja wa kituo cha Michezo mjini Abidjan kujiandaa na michuano ya mchujo wa kucheza kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2012

    Asante blog ya jamii kwa updates.Mimi ndiyo wale wenye roho ya paka.Mimi siamini kama Ivory coast watatufunga 6-0.Kandanda ni mchezo wa maajabu!Vijana chezeni mpira,msiogope majina.Ni bidii tu na kujituma,fuateni maelezo ya kocha.Wapinzani wetu wataingia kwa kutudharau.Uwanja siyo mgeni kwa bahadhi ya wachezaji.Kila la Kheri

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2012

    Hawa wachezaji wetu hivi unavyowaona tu basi wao wenyewe washajuwa kuwa washafungwa tayari

    hawa nikuwapeleka airport wakarudi tu tena ila hapa hamna shauri

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2012

    Tatizo wa TZ hatuna shukurani. Timu ikishinda ooh imebahatisha, ikifungwa ooh tulisema hakuna timu hapo, ikitoa sare ooh timu pinzani iltudharau ngoja mechi ijayo. Nacho ona watu wachache wapiga domo tena wasiyo itakia mema nchi ndiyo wako hiki.KUWENI WAZALENDO NA NCHI YENU.KAMA HAMUWEZI UZALENDO HAMIENI HUKO KWA WANAOJUA KUCHEZA MPIRA,tuacheni sis Wa TZ original.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2012

    Hapa ni kichapo cha mbwa mwizi, mpira hauchezi kwa ulimi, kama ingekua tunashindana kuongea tungeshinda vizuri sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2012

    Ivory Cost watafungwa!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2012

    Ivory Coast 4 vs Tanzania 0

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2012

    KAZENI BUTI MPIRA DAKIKA TISINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...