Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Eng. Suleiman s. Suleiman akiwa na Mh. mwakyembe wakati alipofanya ziara ya kukagua kiwanja cha ndege cha Arusha na kilimanjaro na baadae kuzindua bodi ya ushauri ya KADCO.
akitoa maelekezo kwa Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi dr. mwakyembe,Eng. Suleiman alisema kuwa kiwanja hicho cha arusha kilisimama kupokea ndege kubwa kutokana na ukarabati uliokuwa ukifanyika wa barabara ya kuruka na kutua ndege ambao kwa sasa umekamilika na shirika la ndege la Precision litaanza kutua kiwanjani apo kuanzia mwanzoni mwa July 01 2012.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege alieleza kuwa, mamlaka ya viwanja vya ndege katika mipango yake ya muda mfupi inatarajia kujenga maegesho mapya ya ndege,kujenga jengo jipya la abiria,kurefusha barabara ya kutua na kurukia ndege ili ifikie urefu wa meta 1800 na upana wa meta 30 na kujenga barabara ya kiungio yaani parrarel tax way.
ukarabati ulitakiwa uendelee bila kusimamisha upokeaji wa ndege kubwa.sasa hayo mashirika yaliyositisha kutua KIA ili kusubiri ukarabati, mna hakika yote yatarudisha huduma zao??
ReplyDeleteRafiki ujifunze kusoma vizuri kabla ya kuropoka tu..uwanja unaongelewa hapa ni uwanja wa arusha na sio KIA! Uwanja wa KIA ulikuwa haujafungwa. Na hata kama ingekuwa KIA, kama barabara ya kutua na kuondekea (runway) inakarabatiwa wewe unategemea hizo ndege zingetua wapi?? Jifunze kufikiri kwanza.
ReplyDeleteanonymous wa Jul 02, 06:21,
ReplyDeleteinaelekea hujatoka nje ya tanzania wewe, lakini unajidai mjuaji. tembea ujionee. uwanja wa ndege unapaswa kuwa na runway zaidi ya moja kiasi kwamba ukarabati hausababishi uwanja kufungwa. halafu wale wanaotegemea uwanja wa ndege kwa kipato chao walikwenda wapi, walikula wapi, wakati uwanja umefungwa??
annony hapo juu unaonekana hujui unaloongea,nchi zilizoendelea usifananishe na zinazoendelea,acha kupiga domo wakati hujaifanyia chochote nchi yako kazi kukaa nchi za watu mkija mnataka mkute maendeleo,uliambiwa mashirika ya ndege yanategemea kiwanja kimoja tena cha mkoa ili wale? arusha inapokea domestic flights na sio international,na walikuwa wanatua KIA badala ya pale, nyambafu,unakurupuka tuu,kaoge ulale uko
ReplyDelete