Kaka Michuzi,
hapa ni Stendi Kuu ya Mabasi Singida. Tazama kuna kituo cha polisi, lakini hakuna bendera ya Jeshi la Polisi wala ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! kumbuka, nimepiga picha hii saa tisa alasiri, muda ambao kwa utaratibu bendera inapaswa kupepea!
Ni kama Jeshi la Polisi na Serikali havipo! Haya nimeyashuhudia jana Jumatatu. Sijui kama hili la bendera nalo kweli linatokana na ukata unaolikabili Jeshi letu! Bila shaka huu ni uzembe tu!
Ni mimi mdau,
Manyerere
Manyerere,hii ndio Tanzania bwana,mambo yanajiendea bora kunakucha!
ReplyDeletebondera ipo wapi mdau ??????????? ankali toa hiyo picha inajaza wingi wa habari pasipo na misingi hatuoni bendera hapo.
ReplyDeleteKituo cha polisi bendera sio lazima
ReplyDeletethats right bendera siyo lazima kwa vile tuna mfumo wa vyama vingi si vya chama kimmoja japokuwa ni bendera ya tanzania lakin walio wengi jeshini na polisi ni wa chama cha chinja chawatu milele, ccm
ReplyDeletekuna watu wengine huwa najiuliza hawaelewi au wanajifanya hawaelewi au hawataki kuelewa?Kuna uhusiano gani kati ya kuwa na vyama vingi na kupepea bendera ya polisi ambayo HAIBADILIKI HATA WAKIONDOKA CCM MADARAKANI. AU bendera ya taifa ina uhusiano gani na chama tawala.LET US BE SERIOUS TUNAPOTOA HOJA ZETU.
ReplyDeleteBendera ya Polisi hakuna iliyokuwepo ilisha chakaa kwa mvua ikachanika.
ReplyDeleteOda mpya imetumwa Makao Makuu Polisi Dar Es Salaam, Lori lililobeba mzigo limeharibikia njiani Itigi Mlimani!
Tusubiri kidogo kama vipi kwa kuwa Bendera ya Polisi ni nyeusi, kwa nini kwa muda tusiweke KITAMBAA CHA KANIKI?
Hamuoni mlingoti huo mbele hapo wajameni.
ReplyDelete