Kaka Michuzi, 

hapa ni Stendi Kuu ya Mabasi Singida. Tazama kuna kituo cha polisi, lakini hakuna bendera ya Jeshi la Polisi wala ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! kumbuka, nimepiga picha hii saa tisa alasiri, muda ambao kwa utaratibu bendera inapaswa kupepea! 

Ni kama Jeshi la Polisi na Serikali havipo! Haya nimeyashuhudia jana Jumatatu. Sijui kama hili la bendera nalo kweli linatokana na ukata unaolikabili Jeshi letu! Bila shaka huu ni uzembe tu! 

Ni mimi mdau, 
Manyerere

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2012

    Manyerere,hii ndio Tanzania bwana,mambo yanajiendea bora kunakucha!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2012

    bondera ipo wapi mdau ??????????? ankali toa hiyo picha inajaza wingi wa habari pasipo na misingi hatuoni bendera hapo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2012

    Kituo cha polisi bendera sio lazima

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2012

    thats right bendera siyo lazima kwa vile tuna mfumo wa vyama vingi si vya chama kimmoja japokuwa ni bendera ya tanzania lakin walio wengi jeshini na polisi ni wa chama cha chinja chawatu milele, ccm

    ReplyDelete
  5. kuna watu wengine huwa najiuliza hawaelewi au wanajifanya hawaelewi au hawataki kuelewa?Kuna uhusiano gani kati ya kuwa na vyama vingi na kupepea bendera ya polisi ambayo HAIBADILIKI HATA WAKIONDOKA CCM MADARAKANI. AU bendera ya taifa ina uhusiano gani na chama tawala.LET US BE SERIOUS TUNAPOTOA HOJA ZETU.

    ReplyDelete
  6. Bendera ya Polisi hakuna iliyokuwepo ilisha chakaa kwa mvua ikachanika.

    Oda mpya imetumwa Makao Makuu Polisi Dar Es Salaam, Lori lililobeba mzigo limeharibikia njiani Itigi Mlimani!

    Tusubiri kidogo kama vipi kwa kuwa Bendera ya Polisi ni nyeusi, kwa nini kwa muda tusiweke KITAMBAA CHA KANIKI?

    ReplyDelete
  7. Hamuoni mlingoti huo mbele hapo wajameni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...