Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo Julai 19, 2012 kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya Meli ya Skiget mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haji Khamis, jinsi ulivyandaliwa utaratibu wa kuwahifadhi marehemu watakaokosa kutambuliwa na ndugu zao, wakati Makamu alipofika kwenye Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, leo Julai 19, 2012, kuangalia shughuli za uokoaji na utambuzi wa marehemu. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozio Seif Ali Iddi akizungumza na Wabunge wa Muungano waliofika Zanzibar Kutoa mkono wa pole hapo katika ukumbi wa Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Mbweni kufuatia Ajali ya Meli ya M.V. Skagit.Ujumbe huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua baadhi ya majeruhi wa M.V Skagit waliolazwa katika Hospiotali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Alfonso Lenhardt hapo Serena Inn Hoteli Shangani ambaye yupo kufuatilia raia zake wawili waliokuwemo kwenye meli iliyopata ajali ya M.V. Skagit.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwafariji baadhi ya Watalii na wageni waliokuwa wakija Zanzibar kwa Meli ya M.V. Skagit iliyopata ajali juzi mchana karibu na Kisiwa cha Chumbe. Kulia ya Balozi ni Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Mh. Hamad Masoud Hamad.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema akitoa Taafifa ya uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo Ofiosini Vuga Mjini Zanzibar.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Ali Abdulla Ali akiwa na Makatibu wake wakitoka nje ya Ukumbi wa Baraza hilo baada ya kuahirisha kwa siku moja kikao cha baraza la Wawaklilishi jana asubuhi.Hatua hiyo imekuja kufuatia msiba uliolikumba Taifa baada ya ajali ya Meli ya M.V Skagit iliyozama karibu na kisiwa cha Chumbe.Picha na Saleh Masoud Mahmoud – OMPR-ZNZ.
Much respect kwa viongozi. Dr. Shein,Dr.Bilal,Balozi Seif pamoja na Balozi Merekani Alfonso Lenhardt. Rambi Rambi kwa familia.
ReplyDeleteWakati umeshafika hakuna Imani kwenye serikali ya Rais Kikwete. Hana uwezo wa kusaidia wananchi. Sasa ni wakati wa vijana.Muugano hawna maana tena!
ReplyDelete