Ndugu yangu Michuzi yamenikuta jana jumapili nduguyo. 

Kuna Namba tatu zimetumia utapeli wa hali ya juu kuniliza vijisenti vyangu takriban shilingi laki tatu unusu.Namba zenyewe ni 0717353523 ambayo mpigaji alijitambulisha kama Injinia Emmanuel Shuma lakini amesajiliwa kama Hajji Juma; namba 0716531158 ambayo mpigaji alijitambulisha kama Dr. Andrew lakini imesajiliwa kama AGRO CHEMICAL na namba 0713632239 ambayo mpigaji alijifanya ni raia wa kenya aitwaye Wanjiru lakini amesajiliwa kama Oscar Shuma.

Matapeli hawa wanakupigia na kujifanya wanatafuta dawa ya mifugo inayoitwa GUSTAVIC BEST IN ANIMAL Made in Germany. Kiukweli walinipata lakini nawatahadharisha wadau na watanzania kuwa makini na namba mnazopigiwa na watu msiowafahamu.

Nashukuru Mungu kitengo cha Cybercrime wana taarifa na wanafuatilia na wamenihakikishia kuwa hawafanyi mzaha linapokuja suala la matapeli..

Ndimi mdau niliyelizwa jana jumapili tarehe 15 Julai 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    Hao leo wamenipigia kwa namba tofauti na hizo, wanajifanya wanakufahamu vizuri sana. Dawa wanayotaka ni hiyo hiyo ,bei Usd 3100

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2012

    POLE MDAU LAKINI HILI TANGAZO HALIJAKAMILIKA KANAKWAMBA WALICHUKUAJE PESA KWA VIPI?MDAU REAGING.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2012

    Hivi kuna watu mpaka leo wanalizwa kwa staili hii? Hii kitu ilishafanywa na watu wengi walitapeliwa siku za nyuma. Vyombo vya habari viliandika sana kuhusu utapeli huu lakini kwa vile watanzania hatuna utamaduni wa kufuatilia habari ndo haya yanatukuta.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2012

    POLE MDAU KWA MASAHIBU HAYA .PIA NAMIMI NILIKUTANA NAO PALE ZNZ ILA KWA VILE TULISHASIKIA MCHEZO HUU TULIWAWEKEA MTEGO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MMOJA ALIYELETA DAWA ILI AKABIDHIWE HELA TULIMPATIA VIPANDE VYA MAGAZETI VIKIWA KTK BAHASHA KAMA NDO HELA .TULIMTIA KIBIRU MAKOFI MAZURI NA KUMVUA NGUO KUMBAKISHA NA CHUPI NA KUMKABIDHI KITUO CHA POLISI NGAMBO STATION . TAPELI ALIKUA NA LINE ZA SIM NYINGI PIA ALIKUA NA HERIZI KUBWA TULIPOMUULIZA KUHUSU HERIZI ALISEMA ALIKUA ANAUMWA ALIPEWA NA MGANGA. HAWA MATAPELI WANTUMIA NA UCHAWI KIDOGO LAKINI POLISI HAWAKUWA SERIOUS SANA NA HUYU TAPELI ALIWEKWA SIKU TATU NA KUPATIWA NA DHAMANA INASEMEKANA ALIMTOWA NI KAMANDA MMOJA PALE ZNZ. TULIFANIKIWA KUMPKUTISHA SIMU ZAKE JEANS. ELFU 15000. WADAU TUWE MAKINI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2012

    Uvivu wa kufikir au ugumu wa maisha? Kweli mtu aniibie kizembe hivyo... labda kama wanaroga aisee

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2012

    mimi mwenyewe washanipiga mwaka jana,same story,nina rb.urafiki police...iko siko watapatikana.pole sana mdau

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2012

    MIMI SIO DOKTA WA MIFUGO HALAFU WATU SIWAFAHAMU WANIULIZIE MIMI DAWA YA MIFUGO HALAFU NITOE PESA MFUKONI NIWAPE?LABDA KAMA WANA MAZINGAOMBWE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2012

    Hayo yote yanasababishwa na uvivu wa kutafakari jambo na kupenda mafanikio ya haraka haraka bila kutoa jasho. Kwa ufupi tamaa. Wahenga walisema tamaa mbele mauti nyuma. Ni hayo tu. Tuwe waangalifu wa madili ya mjini.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2012

    Pole sana. Pia nakupongeza kwa ku-share ili wengine wasipatwe. nilimwokoa rafiki yangu mwaka juzi alikua tayari kachukua hela kupeleka, utafiti na maswali kidogo ikaonyesha utapeli. ni ile "Quick Gain"/Return ya biashara ya juu sana kwa masaa ndipo wanakupata. Kumbuka- "If it is too good to be true...."

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...