Ndugu yangu Michuzi yamenikuta jana jumapili nduguyo.
Kuna Namba tatu zimetumia utapeli wa hali ya juu kuniliza vijisenti vyangu takriban shilingi laki tatu unusu.Namba zenyewe ni 0717353523 ambayo mpigaji alijitambulisha kama Injinia Emmanuel Shuma lakini amesajiliwa kama Hajji Juma; namba 0716531158 ambayo mpigaji alijitambulisha kama Dr. Andrew lakini imesajiliwa kama AGRO CHEMICAL na namba 0713632239 ambayo mpigaji alijifanya ni raia wa kenya aitwaye Wanjiru lakini amesajiliwa kama Oscar Shuma.
Matapeli hawa wanakupigia na kujifanya wanatafuta dawa ya mifugo inayoitwa GUSTAVIC BEST IN ANIMAL Made in Germany. Kiukweli walinipata lakini nawatahadharisha wadau na watanzania kuwa makini na namba mnazopigiwa na watu msiowafahamu.
Nashukuru Mungu kitengo cha Cybercrime wana taarifa na wanafuatilia na wamenihakikishia kuwa hawafanyi mzaha linapokuja suala la matapeli..
Ndimi mdau niliyelizwa jana jumapili tarehe 15 Julai 2012


Hao leo wamenipigia kwa namba tofauti na hizo, wanajifanya wanakufahamu vizuri sana. Dawa wanayotaka ni hiyo hiyo ,bei Usd 3100
ReplyDeletePOLE MDAU LAKINI HILI TANGAZO HALIJAKAMILIKA KANAKWAMBA WALICHUKUAJE PESA KWA VIPI?MDAU REAGING.
ReplyDeleteHivi kuna watu mpaka leo wanalizwa kwa staili hii? Hii kitu ilishafanywa na watu wengi walitapeliwa siku za nyuma. Vyombo vya habari viliandika sana kuhusu utapeli huu lakini kwa vile watanzania hatuna utamaduni wa kufuatilia habari ndo haya yanatukuta.
ReplyDeletePOLE MDAU KWA MASAHIBU HAYA .PIA NAMIMI NILIKUTANA NAO PALE ZNZ ILA KWA VILE TULISHASIKIA MCHEZO HUU TULIWAWEKEA MTEGO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MMOJA ALIYELETA DAWA ILI AKABIDHIWE HELA TULIMPATIA VIPANDE VYA MAGAZETI VIKIWA KTK BAHASHA KAMA NDO HELA .TULIMTIA KIBIRU MAKOFI MAZURI NA KUMVUA NGUO KUMBAKISHA NA CHUPI NA KUMKABIDHI KITUO CHA POLISI NGAMBO STATION . TAPELI ALIKUA NA LINE ZA SIM NYINGI PIA ALIKUA NA HERIZI KUBWA TULIPOMUULIZA KUHUSU HERIZI ALISEMA ALIKUA ANAUMWA ALIPEWA NA MGANGA. HAWA MATAPELI WANTUMIA NA UCHAWI KIDOGO LAKINI POLISI HAWAKUWA SERIOUS SANA NA HUYU TAPELI ALIWEKWA SIKU TATU NA KUPATIWA NA DHAMANA INASEMEKANA ALIMTOWA NI KAMANDA MMOJA PALE ZNZ. TULIFANIKIWA KUMPKUTISHA SIMU ZAKE JEANS. ELFU 15000. WADAU TUWE MAKINI.
ReplyDeleteUvivu wa kufikir au ugumu wa maisha? Kweli mtu aniibie kizembe hivyo... labda kama wanaroga aisee
ReplyDeletemimi mwenyewe washanipiga mwaka jana,same story,nina rb.urafiki police...iko siko watapatikana.pole sana mdau
ReplyDeleteMIMI SIO DOKTA WA MIFUGO HALAFU WATU SIWAFAHAMU WANIULIZIE MIMI DAWA YA MIFUGO HALAFU NITOE PESA MFUKONI NIWAPE?LABDA KAMA WANA MAZINGAOMBWE.
ReplyDeleteHayo yote yanasababishwa na uvivu wa kutafakari jambo na kupenda mafanikio ya haraka haraka bila kutoa jasho. Kwa ufupi tamaa. Wahenga walisema tamaa mbele mauti nyuma. Ni hayo tu. Tuwe waangalifu wa madili ya mjini.
ReplyDeletePole sana. Pia nakupongeza kwa ku-share ili wengine wasipatwe. nilimwokoa rafiki yangu mwaka juzi alikua tayari kachukua hela kupeleka, utafiti na maswali kidogo ikaonyesha utapeli. ni ile "Quick Gain"/Return ya biashara ya juu sana kwa masaa ndipo wanakupata. Kumbuka- "If it is too good to be true...."
ReplyDelete