Mkeka wa nguvu maeneo ya Ruvu, mkoa wa Pwani
Baada ya kuchakaa kwa daraja la zamani, hivi sasa barabara kuu ya Morogoro sehemu ya mto Ruvu ina daraja jipya na la kisasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2012

    mkeka mbaya sana lakini hatari ikitokea ajali mdau toka buja

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    ujenzi wa barabara ni gharama kubwa hii lami mswano naomba mainjinia wa fani hii mtujulishe upana wake kwa macho yangu ya sokoni naona tunajenga barabara mpya kwa vipimo vile vile vya zamani yaani nyembamba ajali ndio usiseme kwa vipimo hivi japokuwa udereva wa kasi pia unachangia kwa kasi.
    ikiwa hela ndio tatizo basi ifupishwe urefu lakini ujengaji wa upana huu hatutofikia lengo.
    hili ni wazo tu sio suluhisho.
    salam zao waendesha baskeli usalama wao mdogo.
    mdau.
    Kariakoo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    huu mkeka mbona unaonekana chini ya kiwango.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2012

    huu mkeka haujatulia kabisa yaani una dunda dunda kinoma nadhana ardhi ya hapo haiko fresh kiasi kwamba rami huwa ina bonyea bonyea....mbele kidogo ya hapo kuitafuta chalinze ndo usiseme utazani ngozi ya mzee.....

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2012

    Tukiondoa ufisadi na uvivu tukavaa uzalendo na uchapa kazi yote yanawezekana. Makandarasi wanapunguza vipimo ili kubakisha ten percent, na hii inafanyika kwa baraka za anaelipa kwani nae anapata mgao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2012

    Mkeka wa chalinze mlandizi uko chini ya viwango sana, kwanza barabara ni nyembamba mno. Pili iyo barabara japokua bado ni "mpya" lakini tayari ina bambonde mabonde kama ugali vile. Quality zero.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2012

    Subirini CHADEMA tuchukuwe utawala nyote mtacheka maendeleo kwenda mbele!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2012

    kuna polisi wanakaa hapo ruvu kusimamisha kila gari inayopita na kuwazushia makosa. ni wasumbufu sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2012

    Daraja ni zuri sana ila mmetuzibia tulikuwa tukipita hapo tunauona mto ruvu kwa sasa hauonekani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2012

    Sawa ila...Barabara ni nyembamba sana...eti mkeka wa nguvu! Hakuna hata nafasi ya pembeni ya wanaosafikiri na baskeli au miguu. Daraja nalo ni jemba kama uchochoro wakwenda sokoni kwa miguu...Michuzi tafadhali sana tunakuheshimu....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2012

    Hii njia wala haina muda mrefu na imeshaharibika kabisa. Ukipita na gari ndogo inabidi uibie center otherwise unakita chini. Ujenzi wa halimya chini sana

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2012

    Da da da da mdau amenikumbusha hakuna barabara inatesa kama ya Majumba sita kinyerezi hawakuconsider watu wa miguu kama wanaishi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...