Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Tuvako Manongi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Julai 25, 2012 na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo ulianza jana, Julai 24, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Balozi Manongi ambaye ni ofisa wa miaka mingi wa masuala ya nchi za nje, alikuwa Mshauri Mwandamizi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York.
Balozi Manongi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Y. Sefue ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Desemba 30, mwaka jana, 2011.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
25 Julai, 2012
Hii imekaa vizuri. Balozi Manongi yupo hapo hapo UN kwa hiyo gharama sio nyingi. Halafu bi mkubwa alikuwa hapo juzi ndio amemshauri nini?
ReplyDeleteZanzibar hakuna mwenye akili kwanini watoke bars tu. Udumu Muungano!!.
ReplyDeletewale wale kutoka kitivo cha sheria UDSM
ReplyDeletechaguo lililo bora mhe rais umemteua mtu anaestahili na anaijua UN na mchapa kazi asdiyependa majivuno. mungu ibariki tanzania mungu ibariki afrika.
ReplyDeleteHivi huu msiba wa IKULU kutumia YAHOO EMAIL ADDRESS utaendelea mpaka lini, yaani hakuna kweli mtu mwenye uchungu na nchii hii anayeliona hili au watu wamekalia kuvuta posho na mishahara tu na mawazo mgando bila kuwa na vision yoyote na kazi? maskini nchi yangu Tanzania
ReplyDelete