Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo(kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya msanii huyo na kushoto ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho. John Dilinga, 'DJ JD', nae akiwaeleza wanahabari jinsi alivyotapeliwa na Chameleone mwaka 2005. Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa makini Eric Shigongo. JD akisisitiza jambo (kulia) Juma Mbizo, Mratibu wa Matamasha. Eric Shigongo (kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari. MD wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema leo ameongea na media kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye jana alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza kurejeshewa paspoti yake. 
Eric amefunguka kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo yalikubaliwa. 
Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agenti wa Chameleone ajuliikanae kwa jina la George. 
Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa kweli anawasilina na kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli. 
“Tulipokubaliana nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha, ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba yetu”, alisema Shigongo. 
Akielezea zaidi, Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo fedha. 
“Chameleone alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea advace ya dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine. “Baadae Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti wake, kitu ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na ajenti wake kwetu sisi. 
“Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers, ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege. 
“Ndugu zangu, sikua na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa uchungu. 
Hivyo mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili. 
“Ni dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa kushirikiana na ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye tumeshafanya naye kazi mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni Chameleone ndiye aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo ulikuwa ni mchezo wa pamoja, na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini Kenya. 
“Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,” alihoji Shigongo. 
Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala hili, kwani Chameleone ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya na kubamiza mlango, akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote wapatao miloni 40!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2012

    Nina kaswali kadogo tu: kama huyu jamaa ana historia ya utapeli, kwanini mliingia nae mkataba?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2012

    Poleni sana..Muhaya na Mganda wanakwambieni,,hiyo ni'Magezi ga Baganda',,yaani hiyo maana yake ni akili ya waganda,,siku zote huwaa ni zungusha nikuzungushe,,na bahati mbaya kakutana na hao WaTZ masikini jadi yetu upole,,basi watatuliza sana..Poleni sana!

    I heard!He converted to Islam,how come Still Tapeli(Au mke wake aliendelea kumuwekea mgomo)?
    Ahlam,,London

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2012

    BIG UP SHIGONGO..HUYO JAMAA MPAKA ARUDISHE HIO PESA NDO APATE PASSPORT YAKE SAWA...NO PESA NO PASSPORT NA ASIKANYAGE TZ TENA HUYO MSHENZI...WAGANDA WANA DHARAU SANA WA TZ WAKATI SIE NDO TULIWAOKOA TOKA KWA IDD AMIN...NYAMBAFFF.....GANGAMALA MWANANGU SHIGONGO PESA HIO IRUDI TUU....
    MDAU WA LONDON.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2012

    Waganda wana daharau sana Watanzania, Sioni tatizo la Eric kumnyang'anya Documents zake huyo mvuta bangi. Tena angemchapa na vibao arudi kwao Kuhalalisha Gay marriages rights. Tuacha upole wa kijinga Jamani sisi Wa TZ.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    SAKATA LA CHAMELEON
    Muimbaji chameleon kutoka Uganda ni mwizi sana .Hpa uingereza amesha tapeli watu kishenzi staili hio hio na maneja wake.Ni mchezo wake.Akirudi hapa UK anaweza kupigwa mawe.Bangi zina msumbua tuu.Yeye ninani mtu amabe hawezi kumuheshimu mwakilishi wa Rais wetu Uganda -Balozi wetu pale kampala.Nashanga serikali ya Uganda wamemsikiliza na kuifanya hii ishu itake kuharibu uhusiano mkubwa kati ya nchi hizi mbili.Hivyo chameleone mnamjua ? juzi kawa muislam kesho yake karutadi tena .Bangi haziwezi zina mpelekesha. Anafaa kua jela maana ni msani jambazi.Huko kampala na sikia wamesha rushiana risasi na msani Bobby wine. Naomba watanzania wote tumzomeye chameleon na asirudi tanzania tena kwa tabia yake tena . Hon membe tunaomba hili ulifanyie kazi kwamba wageni hawezi kuja na wakatu abuse hata nyumbani kwetu. Bwana Erik nawe usije uka shika pasport ya mtu ni document ya serikali wala sio mtu binafsi
    Ahsante
    Diaspora writer

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2012

    Eric, tena wala usimruhusu aombe msamaha, wewe mburuze kortini kabisaaaa ili atambue kuna watu wana ustaarabu zaidi na hawapendi wizi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2012

    Shigongo wewe ni mtu ambaye heshima yako iko juu kwa ubunifu na mchango wako kwa jamii, inakuwaje unashidwa kuelewa ni hatua gani ifanyike jambo kama hilo linapotokea?? mbona unatumia mbinu kama zetu ambao hatuna upeo kama wako? Ni sawa na mtu anagonga gari lako barabarani unashuka unachukua briefcase yake na kuondoka badala ya kuchukua number ya gari lake na kusubiri askari wa usalama barabarani. Sheria na taratibu unazijua halafu unafanya mambo kwa ushauri wa ma-bouncer!!! Pamoja na kuwa huyo wanayemuita Dr Chamelion anasemekana ni wa namna hiyo lakini na wewe usingejivunjia heshima kwa kutofuata taratibu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2012

    Jamani tusimuhukumu Chameleone kwa kusikia upande mmoja tumpe nafasi na yeye hawa wote ni wafanya biashara kikubwa watanzania lazima tubadilike hasa ktk ishu ya mikataba lazima tuwe serious kdg tusipoangalia tutatapeliwa kila siku hasa na watu trickery kama kina Chameleone!!!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2012

    Wabongo pia wamezoea kutapeli wasanii, tuwe fair hapa.
    Usanii ni mwigi bongo, na dhuluma.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2012

    sasa hii video yenu mmekatisha sehemu zile nzuri nzuri maanake nini?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 28, 2012

    Suala si Mganda kumdharau Mtanzania, hapa hoja ni Chameleon kutotimiza makubaliano ya mkataba kati yake na Shigongo. Kama amekiuka mkataba basi Shigongo anatakiwa kumdai si tu hizo fedha alizompa bali hata madhara aliyoyapata kwa kuchafuliwa jina la kampuni yake kwa kuonekana tapeli.
    Mdau wa kwanza hapo juu iwe alikua anajua au hajui lakini kama kulikua na mkataba halali na Shigongo alishatimiza upande wa kwanza wa mkataba huku Kinyonga akionesha nia kwa kukubali ofa aliyopewa na kuipokea basi atakua amekiuka makubaliano kwa kutotoa kile chenye thamani ya pesa aliyopokea
    Da haki yako kiongozi ikiwa ni pesa na fidia ya kuchafuliwa

    ReplyDelete
  12. Hivi chameleone amerudi vipi Uganda bila passport?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 28, 2012

    Msilifanye hili ni tatizo la watanzania wote, ni biasahra kati ya two parties. Mazingira yanaonyesha anaweza kuwa tapeli lakini ushahidi hautoshi kuclaim so. Poleni ila nendeni mahakamani na msitumie media kulia.

    ReplyDelete
  14. Poleni sana wandugu !! kwanza huyo msanii kuitwa Chameleon ingekuwa alama ya kukuonya kwamba sio mtu muaminifu, yaani ni mtu wa kigeugeu kama alivyo kinyonga ! leo unamuona kinyonga na rangi ya njano, kesho ya bluu..kuwa macho wakati ukiwa unafanya dili na watu wenye majina ya kigeugeu !! ndiyo maana huyo mganda akajipa jina la kinyonga ili aweze kuwatapeli watu akidhani kwamba kujibadilisha kwake rangi hakutogundulika..!! fala sana huyo mgannda..halafu mshamba sana..waganga kwa ujumla washamba na mimi nashangaa kwanini sisi wa-bongo tunashindwa kuwadhibiti watu local kama waganda....pole kaka shigongo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 28, 2012

    Nina mambo mwaili:

    1. Wewe Sigongo tangu lini ukafanya bishara na wavuta bangi? Kama unafanya biashara na wavuta bangi, hata wewe si mwema, vumilia umeingizwa mjini na mjanja mwenzio.

    2. Suala la watanzania kufanywa wajinga na waganda na wakenya si jambo la ajabu. Ni ujinga wa watanzania ndio unaowafanya watapeliwe. Mbona hata hapa nyumbani mnafanyiwa utapeli mwingi na wabongo wenzetu na mnakubali? nyumbani Mbona sisi wengine tumeishi na hao watu lakini wameshindwa kututapeli. Na sio kwamba hawajajaribu. Ni matapeli kila kona unapowakuta lakini na wewe mtz unapaswa uwe na kili. Usikubali kurubuniwa kirahisi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 28, 2012

    Sasa wenye ufahamu wa sheria naomba mnisaidie; hapa Shigongo anamdai Camelione au anamdai argent wake? Manake watz mnatakiwa mzijue sheria kabla hamjafanya malipo ya kitu chochote. Vinginevyo ikitokea umetapeliwa uwe mpole. Wabongo wameshaibiwa sana kwa kutozingatia sheria kabla ya kulipa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2012

    HAYA NDO MDHARA YA KUSHOBOKEA VITU VYA WENZETU. CHAMELEON SHOO 1 DOLA 8000 + 3500, DIAMOND ALILIPWA DOLA NGAPI?.
    WATANZANIA TUAMKE TUACHE KUFANYWA VITEGA UCHUMI VYA WATU KUJITAJIRISHA KIRAHISI MAANA HIZO HELA SISI NDIO TULIOZILIPA KUPITIA HILO LILILOITWA TAMASHA LA MATUMAINI WAKATI KUMBE NI KITEGA UCHUMI CHA WATU.
    NAYAKUMBUKA MANENO YA YULE MZUNGU WA MAPANKI ALIYESEMA KWAMBA TANZANIA NI NCHI PEKEE KATIKA UKANDA HUU AMBAPO MGENI ANAWEZA KUINGIA BILA SENTI TANO AKATOKA MILIONEA MKUBWA, UTHIBITISHO NI MASHINDANO YA KAGAME YANAYOENDELEA AMBAYO IMEBIDI YAFULULIZE KUFANYIKA TZ KWAKUWA NDIKO MAHALA PEKEE YANAPOLIPA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 28, 2012

    Wote mliotoa comments kuhusu kuwasema waganda mmekosea. Waganda ni marafiki zetu wakubwa mstake kuchanganya issues hapa. Tatizo hapa ni Shigongo na Chamelion. Wadaiane wenyewe wasituingize wananchi wa Uganda na Tanzania kwenye mgogoro wao wa kibiashara. Kwenda kuomba msaada wa kupata Passport yake ubalozini kwetu ilikuwa ni sawa tuu naona, ila kama alidai kwa dharau au alitukana hapo Chamelion anapaswa kupunguza bangi zake. Watanzania tunampenda asitake kuharibu jina lake kwa sababu ya pesa ndogo ndogo au lugha chafu kama ni kweli lakini. Tungependa kupata his side of story too baada ya kumsoma Erick.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 28, 2012

    Eric Shigongo

    Chameleone asipate Pasipoti yake hadi arudishe fedha zote.

    Mtumie nakala za Makataba uliosainiwa na yeye Chameleone Balozi wa Tanzania huko Kampala aone na atoe taafira Polisi huyo mjinga akamatwe.

    Asifikiri waTanzania ni mabwege kiasi hicho.

    Hayo mambo akawafanyie huko Kenya asikoweza kwenda kwa sasa.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 28, 2012

    Huyo Jamaa haelewi ya kuwa Mtanzania ni mtu mpole, mkarimu, mstahimilivu isipokuwa Mtanzania ni mkorofi kama ukiyakanyaga kwake ndicho anachokitaka Chameleone kwetu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 28, 2012

    Chameleone ni Jambazi sana,,,hebu angalia jinsi alivyorudi kwao Uganda bila Pasipoti!

    Sasa mtu wa namna hiyo anasomeka vipi?

    Je, alirudi kwao Uganda kwa Fuso la mbao au Lori la mkaa?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 28, 2012

    Naamini kampuni kubwa kama ya Shigongo ambayo naamini imesajiliwa kihalali haikosi kuwa na Katibu ambaye Kisheria ni Mwanasheria,kutokana na Sheria ya Makampuni ya Tanzania.

    Kwa maana yeye ndie angeona jinsi gani ya kuingia katika mikataba na Mtu kama Kinyonga na sikutegemea aende mtu mwingine katika kusahinisha hiyo mikataba mbali ya mwanasheria.

    Tukiwa tunaingia kwenye mikataba tutumie watu wenye taaluma zinazohusika ili kuepukana na gharama na matatizo yatakayotokana na mikataba ambayo haikushughulikiwa na wataalamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...