Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Nicholas Brooks, akielezea njia nzuri za kuboresha mauzo ya bidhaa za kampuni hiyo,katika mkutano wa kuwapiga msasa mawakala wa mauzo na usambazaji wa vinywaji vya kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Mawakala hao wanatoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Morogoro, Dodoma, Lindi, Pwani na Mtwara.
Meneja wa Huduma za Biashara wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Reginald Mosha akifafanua jambo katika mkutano wa kuwapiga msasa mawakala wa mauzo na usambazaji wa vinywaji vya kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Mawakala hao wanatoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Morogoro, Dodoma, Lindi, Pwani na Mtwara.
Baadi ya mawakala hao kutoka Kanda ya Kusini ya TBL, wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Double Tree, Masaki Dar es Salaam.
Mawakala wakipatiwa zawadi baada ya kumalizika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Nicholas Brooks (wa pili kushoto) akiagana na mmoja wa mawakala. Kulia ni James Bokela ambaye ni Meneja wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Kusini.
Mawakala kutoka Kanda ya Kusini huyo ninaye muona si Anna Kaaya? kama ndivyo please nitafute 0715838899
ReplyDelete