Kwa niaba ya wana-Diaspora wote wanaoishi nchini Canada, Kamati Tendaji ya Zanzibar – Canadian Diaspora Association (ZACADIA) inachukuwa fursa hii kutoa salamu za pole kwa wale wote waliopatwa na maafa wakiwa katika meli iliyozama. Japokuwa tupo mbali na nyumbani lakini roho zetu zipo pamoja nawafiwa wote na majeruhi katika msiba huu mkubwa uliyoikumba nchi yetu.
ZACADIA inawapa mkono wa pole wale wote waliopoteza watoto, ndugu na jamaa zao, na kuwataka wawe na subra kwani hiyo ni miongoni mwa mitihani ya ALLAAH (SW). Tunawatakia afya njema wale wote walionusurika na ajali hiyo.
Mola awalaze mahala pema peponi na awape maghfira waliotangulia katika ajali hii - AMIN!
Katibu
ZACADIA
Toronto, Canada.
Tuko pamoja katika kutoa pole. Mpendwa Nova Scotia
ReplyDelete