Mstahiki  meya wa manispaa ya Songea Charles Mhagama akimshukuru mbunge wa jimbo la songea Dkt Emanuel Nchimbi hayupo pichani mara aada ya kupokea gari ya wagonjwa yenye thamani ya tsh 37 ili iweze kusaidia katika manispaa hiyo,kulia mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkirikiti.

 Mkuu wa wilaya ya songea mkoani Ruvuma Joseph Mkirikiti akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani  ya chama cha mapinduzi juu ya miradi iliyokwisha tekelezwa wilayani humo wakati wa kikao cha mbunge wa jimbo ilo Dkt Emanuel Nchimbi kulia na viongozi wa matawi  wilayani songea,kushoto meya wa manispaa hiyo Charles Mhagama.
 Mbunge wa jimbo la songea mjini ambaye pia ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emanuel Nchimbi kushoto akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya songea Hemed Dizumba wakati wa kikao cha  viongozi kutoka matawi yote ya chama hicho songea mjini.
 Baadhi ya wananchama wa chama cha mapinduzi wakimsikiliza mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la songea mjini na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emanuel Nchimbi  wakati wa kikao kati yao na mbunge huyo katika ukumbi wa songea club mjini humo.
 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emanuel Nchimbi akizungumza na viongozi wa matawi ya chama cha mapinduzi wilayani songea,kulia mwenyekiti wa ccm wilaya Hemed Dizumba na kushoto mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mlirikiti,
 Mwenyekiti wa CCM  wilayani Songea Hemed Dizumba akizungumza na viongozi wa matawi wa wilaya hiyo katika kikao cha kutathimini utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miezi 6 ambacho pia kilihudhuriwa na mbunge wa jimbo hilo Dkt Emanuel Nchimbi

Baadhi ya viongozi wa matawi ya chama cha mapinduzi wilayani songea wakiangalia gari la wagonjwsa lililotolewa na mbunge wa jimbo la songea mjini Dkt Emanuel Nchimbi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa wakazi wa jimbo hilo. PICHA NA MUHIDIN AMRI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mkirikiti za za siku Mheshimiwa? Tulikuwa wote Mafinga JKT Programu ya Chama tena kombania moja!
    Ulikuwa hodari sana wa kukaanga mahindi porini kule IDETERO.

    Mie bwana maisha yananigonga sana na nipo huku Rungemba nakata mkaaa.

    0755660016

    ReplyDelete
  2. Bila shaka ni mkata mkaa wa kisasa/kileo!! Ni wenzako wachache wenye uwezo wa ku'blog'.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...