Wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa wakiwa katika kikao na Maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakati wabunge hao walipofika Ubalozi hapo wakiwa katika ziara ya kikazi na Mafunzo.
Wabunge na Maafisa wa Ubalozi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo ya kupeana taarifa ya kazi na majukumu ya Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kutoka kushoto ni Maura Mwingira, Afisa Ubalozi, Mhe. Vita Kawawa(Mb), Ellen Maduhu, Afisa Ubalozi, Mhe, Edward Lowassa ( Mb) na Mwenyekiti wa Kamati, Dkt. Justin Seruhere, Kaibu Balozi, Mhe. Khalifa Khalifa ( MB) Mhe. Beatrice Shelukindo ( Mb),Meja Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi, Noel Kaganda, Afisa Ubalozi na Rose-Linda Mkapa Afisa Obalozi. Walio simama mstari wa Nyuma ni Modest Mero, Afisa Ubalozi, Alfred Swere, Afisa Ubalozi, Mhe. Rachel Masishanga ( Mb) na Bw. A. Ramadhani Afisa wa Bunge
Wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkutanoni
Kaimu Balozi Dkt. Justin Seruhere akiwa na Mhe. Khalifa Khalifa wakifuatilia majadiliano kuhusu mchakato wa maandalizi ya Mkataba wa Biashara ya Silaha duniani.
Wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"Brigedia Generali , hivi haya majadiliano kuhusu Mkataba wa Sheria ya Biashara ya Silaha Duniani yamekaaje kaaje, hebu tufafanulie ". Ndivyo anavyoonekana kusema Mhe. Rachel Masishanga wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo na Brigedia Generali Dkt. Charles Muzanila kutoka JWTZ ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano unaojadili maandalizi ya mkataba wa biashara ya silaha duniani, kushoto ni Mhe. Beatrice Shelukindo
Mhe. Migiro katika picha ya pamoja na wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ( NUU) ambapo walibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikuwa ni pamoja na kumpongeza kwa kumaliza salama jukumu lake na kueleza kwamba Migiro ni hazina kubwa kwa taifa. kutoka kushoto ni Mama Regina Lowassa, Mhe. Edward Lowassa, na Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro. Waliosimama nyuma ni Mhe. Rachel Masishanga, Mhe. Vita Kawawa, Mhe. Khalifa Khalifa, na Balozi Tuvako Manongi
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, aliyemaliza muda wake, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa katika Picha na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa ( Mb) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wabunge wa kamati hiyo wapo hapa New York katika Ziara ya Kikazi na mafunzo ambapo walipata fursa ya kubadilishana mawazo na Maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na kisha wakahudhuria mikutano iliyokuwa ikifanyika Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Mhe. Migiro akiwa na Mhe, Beatrice Shelukindo


Hivi bunge la bajeti haliwahusu hawa waheshimiwa?
ReplyDelete