Wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa wakiwa katika kikao na Maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa  wakati wabunge hao walipofika  Ubalozi hapo wakiwa katika ziara ya kikazi na Mafunzo.
 Wabunge na Maafisa wa Ubalozi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo ya kupeana taarifa  ya kazi na majukumu ya Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kutoka kushoto ni Maura Mwingira, Afisa Ubalozi, Mhe. Vita Kawawa(Mb), Ellen Maduhu, Afisa Ubalozi, Mhe, Edward Lowassa ( Mb) na Mwenyekiti wa Kamati, Dkt. Justin Seruhere, Kaibu Balozi, Mhe. Khalifa Khalifa ( MB) Mhe. Beatrice Shelukindo ( Mb),Meja Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi, Noel Kaganda, Afisa Ubalozi na Rose-Linda Mkapa Afisa Obalozi.   Walio simama mstari wa Nyuma ni Modest Mero, Afisa Ubalozi, Alfred Swere, Afisa Ubalozi,  Mhe. Rachel Masishanga ( Mb) na Bw. A. Ramadhani Afisa wa Bunge
  Wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkutanoni
  Kaimu Balozi Dkt. Justin Seruhere akiwa na Mhe. Khalifa Khalifa wakifuatilia majadiliano kuhusu mchakato wa maandalizi ya Mkataba wa Biashara ya  Silaha duniani.
  Wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
 "Brigedia Generali ,  hivi   haya  majadiliano  kuhusu Mkataba wa Sheria ya  Biashara ya Silaha Duniani yamekaaje kaaje, hebu tufafanulie ". Ndivyo anavyoonekana kusema Mhe. Rachel Masishanga wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo na Brigedia Generali Dkt. Charles Muzanila kutoka JWTZ ambaye  anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano  unaojadili maandalizi ya mkataba wa biashara ya silaha duniani, kushoto ni Mhe. Beatrice Shelukindo
 Mhe. Migiro katika picha ya pamoja na  wabunge wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ( NUU) ambapo walibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikuwa ni pamoja na kumpongeza kwa kumaliza  salama jukumu lake  na kueleza kwamba Migiro  ni hazina kubwa kwa taifa.  kutoka kushoto ni Mama Regina Lowassa,  Mhe. Edward Lowassa, na Mhe. Dkt.  Asha- Rose Migiro. Waliosimama nyuma ni  Mhe. Rachel Masishanga,  Mhe. Vita Kawawa,  Mhe. Khalifa Khalifa, na  Balozi Tuvako Manongi
 Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa, aliyemaliza muda wake, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa katika Picha na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa ( Mb) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge  ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wabunge wa kamati  hiyo wapo hapa New York katika Ziara ya Kikazi na mafunzo ambapo walipata fursa ya  kubadilishana mawazo na Maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  na kisha wakahudhuria mikutano iliyokuwa ikifanyika Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
 Mhe. Migiro akiwa na Mhe,  Beatrice Shelukindo 
 Mhe. Migiro akiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regine Lowassa.


Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2012

    Hivi bunge la bajeti haliwahusu hawa waheshimiwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...