Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela akizungumza na Mashabiki, Wadau na Wananchi wa Rungwe wakati wa uzinduzi wa Kongamano la kuifufua timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu mkoani Mbeya leo, ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya mpira wa miguu ikishereheswa na ngoma za asili ya watu wa Rungwe ya Ighoma iliyokuwa ikutumbuizwa katika viwanja hivyo, Bonanza lilivuta hisia za watu wengi na wadau wa mkoa wa mbeya na mikoa ya jirani hasa wachezaji waliowahi kuchezea timu ya Tukuyu Star miaka ya 1980 na 1986 huku umati wa watu ukishuhudia tukio hilo. 

Katika bonanza hilo timu ya Rungwe Veterani imefanikiwa kuichapa timu ya wadau wa Tukuyu Star Family magoli 3-1, akielezea mpambano huo Kocha wa timu ya Tukuyu Star Family Kenny  Mwaisabula amesema kushindwa ni sehemu ya mchezo, lakini pia wachezaji wa Rungwe Veterani wako fiti zaidi kimchezo kutokana na kwamba muda mwingi wanafanya mazoezi sana, lakini pia hali ya hewa inawaruhusu kwani wamezoea baridi tofauti na wachezaji wake, Usiku huu kuna kongamano linaendelea mjini Tukuyu ili kujadili mikakati mbalimbali na utaratibu utakaotumika katika kuiendesha Tukuyu Star mpya.


Makamu mwenyekiti wa Tukuyu Stars Family Bw. Peter Mwambuja akizungumza katika bonanza la michezo kwa ajili ya kuhamasisha wadau ili kufufua upya timu ya Tukuyu Star kwenye uwanja wa Tandale mjini Tukuyu leo
Kikosi kizima cha Tukuyu Star Family kikiwa katika picha ya pamoja kulia ni kocha Kenny Mwaisabula Mzazi na kushoto ni Makamu mwenyekiti Tukuyu star Family Peter Mwabuja.
Kocha Koroso naye alikuwepo katika bonanza hilo , Koroso ni mmoja wa makocha waliofundisha mpira nchini Tanzania na nje ya nchi.
Dasi wa Wilaya ya Rungwe Mosess Mwidete akikagua kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kabla ya mchezo kati yake na Tukuyu Star Family.
Ngoma ya Asili ya kinyakyusa inayoitwa"Lipenenga" ikitumbuizwa katika bonanza hilo kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela wa pili kutoka kulia akizungumza mjambo na Mwenyekiti wa kamati ya Kufufua timu ya Tukuyu Star Kenny Mwaisabula, kulia ni Mosess Mwidete RAS wa Rungwe na kushoto ni Peter Mwambuja Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.Picha zaidi  ya tukio hili Bofya Hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hilo si lipenenga, bali linaitwa ling'oma au Ing'oma.

    ReplyDelete
  2. Hivi yule muanzilishi na mdhamini mkuu wa Tukuyu Stars, Kaka (Patel?) yupo hai? Kama yupo hai, mbona hamjamshirikisha? Kosa kubwa sana hilo - yule ndiye alikuwa nguvu kubwa sana nyuma ya mafanikio ya Tukuyu Stars! Yeye na Shafii Bora wa Majimaji ya Songea ndio waliokuwa wadosi wazalendo katika kuleta mafanikio makubwa sana kimpira nyanda za juu kusini.

    Hapa mnataka kufufua Tukuyu Stars na mmemuweka bench mtu muhimu sana - Kaka. Namna gani hii????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...