Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Misewe, Tabata, Dar es Salaam ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika Hisabati na ujumbe ubaoni shuleni hapo jana ikiwa ni mwendelezo wa mgomo wa walimu nchini kuishinikiza Serikali kushughulikia madai yao mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Nini tena mnadai, mishahara si imeongezwa? Rudini mkachape kazi bana. Serikali haina fedha ya kuwalipeni ila ina fedha tu ya kuwaongezea utajiri wanasiasa, watumishi wa TRA na BOT wakiwa duniani. Umeshawahi kusikia wanasiasa, TRA na BOT wamegoma? Siku wakigoma ujue Yesu ameshakuja kwa mara ya pili na kuwanyang'anya utajiri waliopendelewa na serikali.

    ReplyDelete
  2. Mpaka hapo kazi ipo

    ReplyDelete
  3. aaaah..Hii kali aisee!!!!

    Yani mnawalisha sumu watoto wetu. Kha. Heri yenu wenye nazo mnaopeleka watoto shule za st academy...si wa st kayumba mbona watoto wetu wataendelea kuwatumikia wanenu vizazi na vizai kwa mwendo huuu.

    Nimeukumbuka kweli ujamaa

    ReplyDelete
  4. Jamani Mwalimu unatia huruma.........kweli! Unajua unachokifanya au mkumbo?

    ReplyDelete
  5. HATARI KWELIKWELI

    ReplyDelete
  6. Ndio faida ya kutotumia busara kutatua migogoro!!

    ReplyDelete
  7. Wanaoathirika ni watoto wa kimasikini. Hii ni mbaya.

    ReplyDelete
  8. safi sana nimependa hii mafisadi wao wanakula nchi na familia zao na watu wa njee nyinyi mnaoielimisha jamii mnaramba pumba KITAELEWEKA KWELI POA SANA MKUU NATAMANI NINGEMJUA MWALIMU GANI HUYU ILI NIKITUWA BONGO NIJE NIMTUNZEEE

    ReplyDelete
  9. jamani jamani jamani jamani uwiiiiiiiiiiiiiiiiii, seriously? kuna haki na wajibu. siamini kama ninachokiona ni kweli au naota. Hata kama wana haki na wamenyanyaswa kwa kipindi kireeefu bila matumaini ya malipo yao, hiyo adhabu ya kuwajaza ujinga wanafunzi ni mbaya mnooo tena chafu. Najua umuhimu wa mwalimu maana mzazi wangu ni mwalimu, najua ugumu wa maisha tuliopitia kwa sababu ya mzazi wangu kukosa haki zake kama mwalimu lakini bado napinga vikali mnooo kitendo cha mwalimu huyo wa Msewe kuandika upuuzi huo ubaoni. kha!

    ReplyDelete
  10. It's only a fool who can do that. Why do you want to keep a job which doesn't pay? If your employer clearly tells you that they can't afford to pay you more than you are getting, it is opportune time to QUIT.

    Professionals will never scale down the quality of what they deliver, if they remain in their workplace. So, that lady there is only showing how unprofessional and what a BIG FOOL she is.

    If you can read and understand this then know this was not intended for you, for I know you will be a self respecting professional.

    Good night Colleagues.

    Learned Teacher.

    ReplyDelete
  11. Sijui na hasara in ya nani katika sakata hili. Nadhani ni watoto wetu na taifa letu.

    ReplyDelete
  12. Hakutaka jina litajwe wakati sura tunaiona .kazi ipo

    ReplyDelete
  13. Kilishaeleweka maana hata walimu wa primary wengi ni waliofeli form four sasa unafikiri mtafundisha nini zaidi ya 3+3=33. Kazi ipo hadi tukakomboke katika nchi yetu.
    Si kwamba nawasema walimu wa Primary vibaya ila swali langu ni kwamba kwanini watu wenye division four ndo wanaenda ualimu wa primary? nilidhani huko ndo msingi unatakiwa kujengwa kwanini wasiende wenye division one? TAFAKARI NA CHUKUENI HATUA

    ReplyDelete
  14. Huyu mwalimu ajue kwamba watoto wake nao wanafundishwa hivyo hivyo na walimu wenzake!!, bore ugome kuliko kukikuka maadili ya ualimu kwa kuandika vitu visivyo kweli. Walimu nao wanafanya nini darasani kama wamegoma?, muda anaotumia kuandika huo upuuzi ubaoni si angekuwa amewafindisha wanafunzi tayari mambo ya msingi. Aibu kabisa kwa mwalimu kufanya mambo ya kijinga kama haya na hata wazazi na wanafunzi pia!..Gomeni kiustaarabu!

    ReplyDelete
  15. Mlitakiwa mpambane na hao wahusika wakuu na siyo kulipizia kisasi kwa wanafunzi (watoto wetu) ambao hawana hatia yeyote, kuwafundisha kwa mtindo huo ni sawa na kuwaharibia 'future' yao na Taifa kwa jumla.

    Ati hakutaka jina lake litajwe, hovyoooo! Unataka ufichwe moto wakati moshi unafuka mithili moto wa tipper. Jina lisitajwe, si ungeficha na huo wajihi wako basi. Mnapokabiliwa na hali yeyote katika madai yenu, jaribuni kukitafuta chanzo halisi ili muweze kukabiliana nacho na kujuwa tatizo ni nini na lipo wapi ili mtatuwe kwa salama na amani. Fundisha ya namna hiyo kwa ghadhabu zenu haitozaa matunda yeyote. Zingatieni misingi , taratibu na kanuni zenu za ualimu katika kupigania maslahi yenu na sio kukiuka miiko ya ualimu, mmesahau kama huo ni WITO na UTAYARI?

    ReplyDelete
  16. Mnataka mishahara mikubwa wakti wanafunzi mnaofundisha wanamaliza la saba wengi hawajui kusoma wala kuandika? mshahara mkubwa kwa elimu gani mliyonayo? form four division four point 28. Mmependelewa sana kupewa hiyo kazi. Ingieni darasanj na muwe na adabu, kama mshahara mdogo acheni kazi.

    ReplyDelete
  17. Research zinzonyesha kuwa walimu wakipewa pesa nyingi zaidi especially wa vijijini ndo kitakuwa kiyama cha elimu usidhani serikali ni kichaa kwani kila anaetoka vijijini ataniambia pindi neema inapowatembelea inakuwaje.ULEVI KWA WINGI

    ReplyDelete
  18. Nishasema labda mbingu zishuke ndo bongo itaendelea, hapo watoto watakula sumu hadi wakae sawa huku watoto wa mafisadi wanasoma fresh na ikibidi nje ya nchi. Ni kizazi hata kizazi tajiri atakua tajiri na masikini ataendelea kua masikini hata bible ilisema mwenye nacho ataongezewa na asienacho hata kile kichache atanyang'anywa.

    ReplyDelete
  19. what kind of teaching is this?, huyu mwalimu inatakiwa ashitakiwe kabisa, hata ukidai haki yako unafundisha upuuzi namna hii?,hata sisi wazazi tunaku-support vipi sasa?,walimu siku ni kuwa na heshima sasa kwa mtindo huu taifa litakuwaje?,huyu mwalimu anaonyesha upuuzi anaofundisha watoto wetu na kudai pesa zaidi, haiwezekani. mwalimu mwingine mpuuzi kama yeye anamfundishia mwanae hivyo hivyo kama hajui.

    ReplyDelete
  20. Huyu anauhakika hata akifukuzwa hapo atapata kazi St. Mary's, filbet bayi primary, st.anne maria, feza etc...hata kabla ya nyongeza hivyo ndio anavyofundisha so ameonyesha ukishoka wake kwa watanzania wote.

    Lakini kama mtaalamu, mwajiri akisema unachotaka sina unamlazimishaje? Hili soko huru nenda kunakolopa hizi ni dalili za kutokuwa na mbadala.

    ReplyDelete
  21. Che GUevaraAugust 04, 2012

    Kusema kweli walimu wa Tz hasa Primary wametupwa sana! kwanini wao wapewe mshahara mdogo na wabunge wapate milioni 11 kwa mwezi? wao hawana mahitaji? msiwatishe acha nao wadai haki yao na kama sisi wazazi tunapenda maendeleo ya watoto wetu TUWAPIGANIE walimu kwanza

    ReplyDelete
  22. Mimi sioni kosa kwenye haya mahesabu, ni sawa tu anachofanya mwalimu, eti watu wa sociology, political science, Law, anthropology, linguistic kuna kosa hapa?

    ReplyDelete
  23. Zamani tulikuwa tukisikia kwamba ualimu ni wito hivyo sio kwamba ni kazi anayoweza kuifanya kila mtu lakini siku hz wanaoingia ualimu ni wale wanaokwenda ili mradi kufanya kazi na kupata pesa sasa hapo tunategemea nini??? walimu wengi wakishahitimu huo ualimu hawapendi kuendelea tena kusoma yaani kujiendeleza sasa mnapowaambia waache kazi watakwenda wapi??Nafikiri umefika wakati hata serikali kubadilisha mfumo ya jinsi ya kuwapata waalimu wa kufundisha hawa watoto wetu....

    ReplyDelete
  24. Mwalimu hivi wewe ulipokuwa unasoma uleisomeshwa mahesabu ya ndivyo sivyo kama hapo?

    Hili ni tatizo kubwa sana kwa kuweka Waliofeli kuwa ndio katika Sekta ya Ualimu.

    Hivi Chuo Kikuu au Elimu ya Juu wanaofundisha wamefeli huko nyuma?

    Mchawi wa Elimu yatu kushuka ndio ktk hili,unakuta mtu yupo Sekondari kuandika jina lake ni tabu na jina lenyewe kaandika kwenye sehemu ya tahere!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...