Leo ni Hepi Besdei ya Kuzaliwa mtoto Sellah Muhidin (kati, kaka yake Booby na rafikiye) naye akaamua akasherehekee na wanafunzi wenzie wa shule ya Lady Chesam Nursery School iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam. Sellah, ambaye anatimiza miaka 3,  ni mtoto wa mwisho wa Ankal ambaye alialikwa pia katika kamnuso hako ambako hakukafaidi kutokana na swaumu.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. ankal una wangapi? Au na wewe hujui kama naibu spika?

    ReplyDelete
  2. Happy Birthday Sellah.

    Michuzi, inabidi ufunge kamba au umfunge kamba, uzazi unakwenda na umri. Mungu akupe maisha ya kumwoma Sellah chuo kikuu ukiwa na umri wa miaka ....75?

    ReplyDelete
  3. They are so angelic. God bless Sellah. Hongera Ankal kwa malezi mazuri na kwa kumwekea misingi bora.

    ReplyDelete
  4. Ankal,
    Hongera bana. Huyo binti ni Sellah M. Michuzi. Kwa utambulisho mzuri hiyo M. inabidi kuiweka kapuni na kubaki na Sellah Michuzi.
    Aise, wa mwisho? Maana yake ni wa ngapi?

    ReplyDelete
  5. Ankal inamaana Sellah na Bobby hawajauona? hahaha

    ReplyDelete
  6. Happy Birthday Sellah..be blessed with many many more..

    ReplyDelete
  7. Eti wa Mwisho.. he he he!!... Acha mashara ankal!!!..

    HBD Sellah

    ReplyDelete
  8. Wa mwisho maana yake umemaliza au ni kwa sasa?

    ReplyDelete
  9. Very cute babies!! HAPPY BDAY!!1Ni wa mwisho kwa sasa au ni wa mwisho kabisa?

    ReplyDelete
  10. Ankal mchoyo, vikeki viwili tu jamani ?

    ReplyDelete
  11. Ankal now umekuwa babu bwana, acha sasa, sellah anapendeza kweli kuwa mjukuu wako

    ReplyDelete
  12. Mdau wa pili kutoka juu unayesema wakati sellah atakuwa chuo kikuu Ankal atakuwa na Umri wa miaka 75,Lakini ukumbuke kuwa Ngombe azeeki maini,mhh..Ankal safari bado unazo ndefu

    ReplyDelete
  13. Ankal naona bado humo,ilo Gap limetulia,mbona hatumuoni mdogo wake sellah.

    Nursery school - 50:3 Ankal:sellah
    Univesity - 72:25,Ankal:sellah

    Nakutakia besidei njema sellah

    ReplyDelete
  14. Sema Bro Michuzi mzee wa kazi,kofia ya Olimpiki nini?.

    1.Mpe hongera sana Sellah
    2.Mwulize kama yuko tayari nilete posa,posa yangu ni Ice cream na keki tu kama anatumia.
    3.Kizazi hiki kinaweza kuifaidi nchi yetu manake naona tunaelekea ''kwenyewe'

    David V

    ReplyDelete
  15. Huyo ni mtoto mdogo wa Ankal na wala sio wa mwisho, mwandishi ana uhakika gani kuwa Ankal hana uwezo wa kupata mtoto mwingine?. Hongera mtoto.

    ReplyDelete
  16. Asalaam alaykhum ankal, namtakia maisha marefu mema yenye furaha pamoja na afya njema ankal Sellah amiin.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  17. Ankal!Umejuwaje ni wa mwisho,,Mimi nahisi ni wa kati,,Insha'Allah wengine wanafollow!
    Mansha'Allah Sellah ni Kaquite na hao wenzake pia.Allah awakuzieni watoto wenu kwa maadili yaliyomema!Na sisi pia wakwetu Insha'Allah tukija'aliwa!
    Ramadhan Mubaraqa Michizi's Family!
    Ahlam...London

    ReplyDelete
  18. Kaka,

    Inakuwaje! Mtoto wa miaka mitatu umri huo? Me nilidhani alitakiwa awe Mjukuu yaani mtoto wa yule binti yako uliyeendaga kwenye Gradueshen yake kule shule ya Babros sijui vile!

    Mweeh,

    ReplyDelete
  19. Happy Birthday Sellah me na your sister Natasha tunakutakia maisha marefu na Mungu akukuze,love u mwa!

    ReplyDelete
  20. Ankali kwenye status yako flani ya facebook uliandikaga uko single sasa hao watoto ndugu yangu, mama wangapi? Inshallah wasomeshe vizuri

    ReplyDelete
  21. Happy Birthday Sellah.

    ReplyDelete
  22. Mama yake na huyo mtoto yuko wapi? Men????? Sina hamu! Kwenye chumba cha uzazi (labor ward) ni mama anayehangaika kumleta mtoto duniani, lakini kwenye sherehe za kutimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa....baba ndie yuko mbele mbele...... Please Ankal, kama mamake yuko katika hizo picha, mtambulishe tafadhali.......otherwise, itakupunguzia value hasa kwa wadau wako kina mama, kama mimi!

    ReplyDelete
  23. Ankal,

    huyo ndo wa mwisho kweli au?

    ReplyDelete
  24. Mashallah, watoto wamependeza, Michuzi hii usiibane nakuomba umfikishie aliyeandika yale maneno pale ubaoni. Kwanini kama hajui kingereza asitumie kiswahili, lugha yetu ya taifa ambayo pia hata wengine humu hawaijui na wanakimbilia kingereza. Sherehe ya mtoto na wenzie ni nzuri sana imependeza kasoro ni lile neno la kuzaliwa lililokosewa spelling. limeboa sherehe na atawamislead watoto. kwani hii shule ya chekechea haifundish kiinglish?

    ReplyDelete
  25. Hongera kwa Sellah Inshallah Allah SW amkuze vyema!

    ReplyDelete
  26. Tuacheni masihara!

    1.Mambo ya majaaliwa ya uzazi,
    2.Urefu wa kuishi maisha,
    3.Hatima ya maisha yetu kama la utajaaliwa kumwona mwanao ktk umri fulani,

    Yote hayo matatu (3) na mengine tusiyoyajua ni mipango ya Mungu!

    TUACHE USHIRIKINA NDANI YA MWEZI MTUKUFU KWA KUMWINGILIA MWENYEZI MUNGU KTK MAMLAKA YAKE!

    ReplyDelete
  27. Mjomba Uchumi unauweza!

    Nimekuvulia kofia, kwa ukwasi ulio nao wa ziada umefanya kitu simple tu.

    Utawajibika kutoa Semina Elekezi kwa ndugu zetu wengine wanaotumia fedha ndeeefu kwa Sherehe bila malengo!

    ReplyDelete
  28. Uratibu wa maisha unafanywa na Mwenyezi Mungu.

    Mbona wapo waliozaa na kufa wakiwa wangali vijana wabichi chini ya miaka 30 wakawaacha watoto wakiwa wadogo?

    Je, hao walimkosea Mungu?

    Hivyo suala la Ankali kumwona bintiye akiwa Chuo Kikuu huku yeye akiwa at 75 hiyo ipo chini ya Mamlaka ya Mungu pia.

    ReplyDelete
  29. Huyo anayedai uzazi unakwenda na umri kilaza kweli kweli.

    Ina maana unataka kuwahakikishia watu kuwa Babu yako wa miaka 75 kama uwezo wa kijinsia anao hawezi kukujazia mimba mkeo?

    Mkumbuke ya kuwa uwezo wa kijinsia ni tofauti na uwezo wa kimwili hasa kwa wanaume hata mwenye umri wa miaka zaidi ya 75 anaweza kizalisha!

    ReplyDelete
  30. Ohhh umri wa mzazi na mtoto hauendani!

    Mnataka kutueleza wengine mnayo mawasiliano na Mungu?

    ReplyDelete
  31. Mnhhh

    Acheni kujivika Koti la Mwenyezi Mungu kwa kumpangia Ankali majaaliwa ya kimaisha!

    Kila kitu ni siri ya Mungu.

    Ni nani ajuaye kilicho mbele yetu sote?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...