Picha na HAbari Na Dixon Busagaga Busagaga 
wa Globu ya Jamii Moshi.

KAMPUNI ya Megatrade Investiment Ltd kupitia kinywaji chake cha K-Vant Gin imeamua kuidhamini timu ya mpira wa miguu ya Polisi Kilimanjaro ili kufanikisha ushiriki wake katika ligi ya mpira wa miguu ya Polisi jamii mkoa wa Kilimanjaro. Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu hiyo,meneja mauzo na masoko wa kampuni hiyo Goodluck Kway amesema hatua hiyo ni mipango ya Megatrade kurudisha faida kidogo inayopata kwa jamii kupitia njia ya michezo.

Amesema kwa kuthamini michezo ,mchango wa jeshi la polisi katika ulinzi na usalama wa raia pamoja na dhana nzima ya ulinzi shirikishi au polisi jamii kampuni hiyo imeamua kudhamini timu hiyo ili kuongeza hamasa katika mahusiano baina ya askari polisi na raia. Kway alisema vifaa vilivyotolewa vinathamani ya kiasi cha shilingi milioni 6 ambavyo ni seti moja ya jezi,viatu jozi 18,glovu za mlinda mlango seti mbili,mipira 4,vizuia ugoko seti 18 na suti za michezo.

"Ni matumaini yetu kuwa vifaa hivi vitaongeza hamasa katika ushiriki wenu katika michezo hii na pia mtakuwa mabalozi wazuri wa kinywaji cha K-Vant"alisema Kway. Kwa upande wake kamanda Boaz ameishkuru kampuni ya Megatrade kwa msaada huo na kwamaba umekuja wakati muafaka wakati jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro likijiandaa kuirejesha timu  yake katika medani ya
soka baada ya kupotea kwa takribani miaka 5.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya kiasi cha sh,milioni 6 kwa timu ya soka ya Polisi Kiliamnjaro.kushoto kwake ni meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd Goodluck Kway .
 Mchezaji wa timu ya polisi Kilimanjaro Atwai Omary akiwa katika uzi mpya wa timu hiyo ,baada ya kukabidhiwa na kampuni ya Megatrade Investment Ltd,jezi hizi zinataraji kuanza kutumiwa wakati wa ligi daraja la nne ambayo inataraji kuanza Septemba Mosi mwaka huu.
 Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd Goodluck Kway akimkabidhi kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya Polisi Kilimanjaro.
Kocha wa timu ya soka ya Polisi Kilimanjaro Issa Lugaza akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vifaa hvyo na kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mchezaji usingizi bwaaaa, au tayari kamaliza chupa zima la gin. Duh !!! kweli iko siku tutalinyakua kombe la dunia ,lakini kabla ya hapo, wacha kwanza tukate maji.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  2. safi sana megatrade nawaamini, mnafaa sana heshima yako Francis Kimaro mwenye kampuni ana roho nzuri sanaaaaaaaaaaaaaa hana makuu,hongera sana kaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...