![]() |
| Kikosi kizima cha Tukuyu Star Family kikiwa katika picha ya pamoja kulia ni kocha Kenny Mwaisabula Mzazi na kushoto ni Makamu mwenyekiti Tukuyu star Family Peter Mwabuja. |
![]() |
| Kocha Koroso naye alikuwepo katika bonanza hilo , Koroso ni mmoja wa makocha waliofundisha mpira nchini Tanzania na nje ya nchi. |
![]() |
| Dasi wa Wilaya ya Rungwe Mosess Mwidete akikagua kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kabla ya mchezo kati yake na Tukuyu Star Family. |
![]() |
| Ngoma ya Asili ya kinyakyusa inayoitwa"Lipenenga" ikitumbuizwa katika bonanza hilo kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali ya mpira wa miguu. |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh. Crispin Meela wa pili kutoka kulia akizungumza mjambo na Mwenyekiti wa kamati ya Kufufua timu ya Tukuyu Star Kenny Mwaisabula, kulia ni Mosess Mwidete RAS wa Rungwe na kushoto ni Peter Mwambuja Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.Picha zaidi ya tukio hili Bofya Hapa. |









Hilo si lipenenga, bali linaitwa ling'oma au Ing'oma.
ReplyDeleteHivi yule muanzilishi na mdhamini mkuu wa Tukuyu Stars, Kaka (Patel?) yupo hai? Kama yupo hai, mbona hamjamshirikisha? Kosa kubwa sana hilo - yule ndiye alikuwa nguvu kubwa sana nyuma ya mafanikio ya Tukuyu Stars! Yeye na Shafii Bora wa Majimaji ya Songea ndio waliokuwa wadosi wazalendo katika kuleta mafanikio makubwa sana kimpira nyanda za juu kusini.
ReplyDeleteHapa mnataka kufufua Tukuyu Stars na mmemuweka bench mtu muhimu sana - Kaka. Namna gani hii????