MCHUNGAJI KRISTOFA HENERI DAUD MAHIMBO
22 APRILI 1929 – 06 AGOSTI 2011
Isaiah 57:1-2
Masaa, Siku, Wiki, Miezi na sasa ni mwaka mmoja tangu Mungu wetu mwenye wingi wa rehema na upendo alipodhihirisha utukufu na mapenzi yake makubwa kwako hadi akaamua kukuchukua alfajiri ya siku ya Jumamosi terehe 06/08/2011. Huzuni na majonzi bado vimebaki kuwa ni sehemu ya maisha yetu katika familia lakini tuna imani neno la Mungu litatimia na siku moja tutakutana tena; na hapo hatutatengana tena milele. Matendo yako mema yamebaki kuwa lulu na mwanga uiangaziayo familia yetu. Maisha yako ya upendo, unyenyekevu, uadilifu, utu wema na bidii katika kazi ndiyo dira inayotuongoza sisi, mke wako Brenda, watoto wako Godwin, Annette, Dorothy, Huruma, Upendo, Florence, Aidan na Martha na Neema na Rehema, wakwe zako Michael Simukanga, Albert Mazuki, Ladislaus Matindi, Rehema na Demitria pamoja na wajukuu zako wote. Tutakukumbuka sana na kukulilia siku zote. Tunaendelea kukuombea ili upate pumziko la amani milele na milele.
Unakumbukwa sana na wadogo zako William, Anna, Sabina na Maria, wapwa zako, ndugu wa ukoo wa Mwegoha na familia zao na ndugu wengine wote pia. Kwetu sote imebaki kumbukumbu ni jinsi gani ulikuwa mhimili wa familia. Unakumbukwa pia na Wachungaji wenzako, rafiki zako wana Yanga, wanasiasa wenzako na ndugu na jamaa wengine wengi ambao bado wanakumbuka bidii yako na mchango wako mkubwa ulioutoa katika kulitumikia Taifa hili. Bado wanazungumzia hulka yako ya uaminifu, uadilifu, unyenyekevu na kupenda haki viliyokujengea heshima kubwa miongoni mwa jamii.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.
“Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake.” 1 Wathesalonike 4:13-14



pole sana upendo,mpe mama pole na ndugu wote.
ReplyDeletefrm Suma USA
Poleni sana wapendwa
ReplyDelete