Jumapili iliyopita nilizungumia umuhimu wa kupata na kuhifadhi kumbukumbu kwa njia ya picha, hususan kwenye matukio ya kihistoria kama ya Olimpiki, ya wanamichezo wetu wakiwa katika michuano hiyo kwa faida ya vizazi vya leo na kesho.
Mada hiyo ilitokana na ukweli kwamba sisi wa-Tanzania hatuna utamaduni wa kutuma mtu ama watu wa kuweka kumbukumbuku hizo adhimu, tukitegemea tu mashirika ya habari, ama picha mbili tatu zinazopigwa na wanamichezo wenyewe ama viongozi wao ama marafiki kwa ajili ya albamu binafsi badala ya rekodi za kitaifa ambazo ni muhimu kuwa nazo.
Nashukuru kwamba wengi waliafikiana nami, na wengi zaidi walitoa maoni kwamba kasoro hiyo lazima ifanyiwe kazi, vinginevyo tutajikuta hatuna kumbukumbu ya wanamichezo wetu wakiwa ulingoni.
Wadau wengine walikwenda mbali zaidi, kutaka kujua mbinu mbalimbali za kuhifadhi picha, ikizingatiwa kwamba siku hizi wengi wetu hutumia kamera za digital, na mahali pekee pa kuhifadhia wengi wanajua ni katika kompyuta zao tu.
Na hii ndio mada yangu ya leo; kuzungumzia njia mbalimbali za kuhifadhia taswira zetu, ikizingatiwa kwamba faili za picha za digital ni kubwa mno kiasi ya kwamba haichukui muda nafasi katika kompyuta hujaa haraka, na kumfanya mtu ahangaike na asijue la kufanya.
Hapo kazi yako inakuwa ni kukusanya mafaili yako yote na kuyahifadhi humo. Kisha, hata kama utasafiri, popote pale penye intaneti utaweza kufungua anuani yako kwa jina na password (kama ufanyavyo wakati wa kufungua akaunti yakeo ya email) na kutumia mafaili yako wakati wowote na mahali popote palipo na intaneti.
Kama nilivyosema, zipo njia nyingi mithili ya hiyo Dropbox, ila naitaja hii kwa kuwa ni rahisi na yenye uhakika kiasi.
Mie mwenyewe nimekuwa nikiitumia kwa muda sasa, na sijajuta. Yaani mambo ya kubeba ma CD ama ma DVD ama hata hizo External Hard drive nimeshayasahau kitambo. Maktaba yangu ya picha ipo hewani ama ‘mawinguni’, na popote nilipo, mradi kuwe na intaneti, naweza kuita mafaili yangu yote na kutumia yaliyomo. Adha ya moto, wizi ama kuharibika kwa kifaa cha kuhifadhia inakuwa haipo tena.
Uzuri mwingine wa kutumia njia hii ni kwamba endapo mtu atataka umtumie picha ni kwamba wewe kazi yako ni kufungua akaunti yako ya Dropbox, ama inayofanana nayo, kisha unatuma kwa email kupitia humo humo kwenye anuani yako. Na kama hata yeye unayemtumia atakuwa na akaunti hiyo ya Dropbox, kazi inakuwa rahisi zaidi.
Ila tu ikumbukwe wenzetu wanatoa huduma za namna hii kibisahara. Kwa hiyo ukitaka kupata nafasi kubwa zaidi katika akaunti ya Dropbox yako inabidi ulipie kiasi, japo kwa kuanzia wanakupa ofa ya bure ya nafasi kiasi cha GB 100 hivi… Bei aghalabu si ya kutisha. Utakuta unatakiw kulipa kati ya dola 20 hadi 100 kwa mwaka, kulingana na mahitaji na uwezo wako.
Namna ya kulipia huduma hizo pia sio ya kusumbua kama unavyoweaza kudhania. Wewe kama una akaunti katika benki inayotoa huduma kama vile za Visa ama Mastecard, unaweza kununua nafasi ya ziada kwa njia ya mtandao. Nenda hapo benki ukaisajili kadi yako iunganishwe kwenye huduma ya manunuzi mtandaoni, nawe unaweza kufanya manunuzi mara moja. Fuata maelekezo ya hapo benki na yaliyo katika akaunti yako nawe utafanikiwa tu.
Njia zingine, kwa mfano wale wenye kutumia vifaa vya Apple, kama vile kompyuta, ipad na iphone, ni ile inayojulikana kama iCloud, ambayo akaunti yake pia huweza kutumika kwenye kompyuta zingine pia.
Kazi yake nayo ni ile ile ya kuhifadhi mafaili yako ‘kwenye mawingu’. Yaani bila kuwa na haja ya kubeba vifaa vya ziada. Na hii pia unaanza kwa huduma ya dezo, nawe ukitaka nafasi zaidi unachangia uchakavu kidogo.
Natumai nimeeleweka kwa hilo, na mwenye maswali zaidi anaweza kuuliza tu, ama hata kutoa mwongozo zaidi ili wadau mnufaike. Pia jaribu kuwa mtundu wa kucheza na google na kusaka huduma za kuhifadhia mafaili kwa njia ya mtandao.
Naomba kuwasilisha;
-Ankal

Ankal vipi,FUFU limekulewesha hadi umechelewa kuweka mada..?Asante Ankal,drop box nilikuwa nahifahamu sana ila sikujua kama unaweza kuitumia kwa kutunza mafaili makubwa kiasi hicho.Na umeandika kama mwandishi uliyebobea kweli kweli,haichoshi kusoma..kila nilipomaliza paragraph nilitaka kurukia inayofuata haraka.Kila ulichosema nilidhani ndiyo suluhisho kumbe kuna kingine chini yake!!
ReplyDeleteDavid V
Nilidhani leo umetusahau au fufu la Ghana limekulevya.
ReplyDeleteAhsante sana hii dropbox kwa kweli sisi wengine ndio mwanzo tuisikie kutoka kwako. Tunashukuru kwa taaluma.
Ujumbe umetufikia.
Asante kweli shule ya bure. Kweli mwisho hauna elimu!
ReplyDeletehttps://drive.google.com/start#home
ReplyDeleteHere you get 5GB free, it is not like the 2gb of dropbox
dropbox na Icloud sio teknolojia za kushabikia. Hata muasisi wa Apple alilia akipinga utumiwaji wa Icloud sasa wewe mwenye kupigia debe inaelekea hujajua maana ya data confidentiality. kama una computer yenye gigabyte 500, sidhani kama unahitaji internet kuhifadhi faili zako hata siku moja hao dropbox ambao mafaili yako ukiyaweka yanakuwa mlango wazi kwa wenye kujua nini maana ya internet hawawezi kukupa gigabyte 500 za bure. kama waungwana mjuavyo "BURE GHALI" AMA CHEAP OR FREE IS EXPENSIVE BUSINESS. Kwa hiyo mimi kama mtaalam wa mambo ya computer sishauri mtu aweke faili lake kwenye dropbox ama icloud.
ReplyDelete