Mbunge wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto (kulia) akitoa maelezo binafsi kwa waandishi  wa habari leo,  kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yake hususan kuelekea katika kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati. Kushoto ni   Mbunge wa Bukombe, Prof Kulikoyela Kahigi (CHADEMA). 
Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

Ndugu Waandishi,
Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote  zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.
Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hata mi nilikuwa na shaka kuwa zitto anahusishwa kwa kuwa alitetea utaratibu.Watanzania mkimweka rehani Zitto nchi imekwisha.Inawezekana Kweli Muhongo alikiuka na ikawa kwa nia njema.ila kwa kuwa na zito hakujua nia yake njema basi uchunguzi uishe tuwe na amani.kazi ya zito haina shaka ila akikutwa na rushwa tutamtosa.

    ReplyDelete
  2. kama kweli hujakula mlungula fungua kesi ya madai kuchafuliwa jina. dai bilioni 10 shs. rushwaaaaaa mpaka kupitisha hoja bungeni mnashangaaa. mama ntilie hatoi kijiko mpaka umshikishe vinginevyo utakula na mkono na maji hatoi...nunua uoshe nkono wako.

    ReplyDelete
  3. NDIYO UMEKULA, USILE SI UTAKUFA UNAFANYA MCHEZO NINI. NJAA INAUA. SEMA NIMEKULA NA NINENDELEA KULA ILI NIISHI. HATA HAO WANAOKUSEMA WANAKULA PIA. KULA NI UHAI NA UHAI KUNAHITAJI KULA

    ReplyDelete
  4. Nasema hiviii! chembe ya rushwa imeota akilini mwa Watanzania. hakuna hata mmoja nayetaka madaraka kwa manufaa ya taifa bali naona tu wote ni maneno mengi katika harakati za kujichotea haraka haraka kabla muda kwisha.
    Kila siku watu wanalalama huduma mbaya! utendaji mbaya yuko wapi aliyesuluhisha hili.
    Wahenga walisema "Maneno matupu............."

    ReplyDelete
  5. Hii tabia ya kuzushiana mambo mmeianzisha nyie wentewe CDM, sasa unalalamika nini, na hivyo ulivyotangaza kugombea urais utaandamwa mpaka uonekane haufai mbele watanzani,nashukuru mungu wewe mwenyewe umegundua kuwa uzushi huu umesambazwa kimkakati, hasa kwa upande wa CDM wenyewe.

    ReplyDelete
  6. Wewe una kosa moja tu la kutaka kugombea Urais halafu ni wa dini fulani, watu wameapa kwamba huyu ni raisi wa mwisho wa dini hiyo. Halafu mkoa unaotoka wengi tunaambiwa si watanzania tu ila na wewe hutoki ule mkoa wanakotoka wenzako wanaotoka kujitenga kama sudan ya kusini. Kigoma kuna madini au mbuga maarufu za wanyama. Mwaka 2015 tutakuwa wahindi, wakati wa uchaguzi tunaenda holiday maana hapatakalika.

    ReplyDelete
  7. Zitto, huyo binti wa nyuma mwenye kilemba anafaa kuwa mchumba wako!!! She's so beautiful, heheh.

    ReplyDelete
  8. BARUA YA WAZI KWA ZITTO KABWE......

    HATA MIMI NAHISI UMEKULA PESA WEWE ZITTO KWA SABABU NGUVU UNAYOTUMIA KUBISHA NI SAWA KABISA NA ILE YA EZEKIEL MAIGE, NASHANGAA KINACHO KUFANYE UWE NA SIMANZI KWANI NANI HALI RUSHWA TANZANIA? KILA MTU TANZANIA KATOA AMA KUPOKEA RUSHWA KWA NJIA MOJA AMA NYINGINE, HUU NI UTALATIBU TULIO UZOEA ILI MAMBO YAKUENDEE POA UNATOA CHOCHOTE, TUNAFANYA HIVI POLISI BARABARANI KWA TRAFFIC VYUONI HOSPITALINI BANK KWENYE KUPATA KAZI KUSAFIRI KUMPATA DEMU KUSHINDA MISS TANZANIA KUPANGWA KWENYE TIMU NA SASA BUNGENI KWENYE KESI MAHAKAMANI KWA KIFUPI RUSHWA NI PART OF OUR LIVES. NAKUSIHI KAKA YANGU ZITTO WA KABWE USIVUNJIKE MOYO WEWE TAFUNA HIYO PESA MPAKA PALE ITAKAPO KOSEKANA HUJUI MUNGU KAKU PANGIA NINI KESHO. NARUDIA TENA RUSHWA NA MAISHA YETU NI KAMA COMPLIMENTARY DEMAND VINA KWENDA PAMOJA KAMA CHAI NA SUKARI.

    ReplyDelete
  9. Chadema wamekanusha hadharani kuwa Zitto anahusika na rushwa ila wametaka uchunguzi ufanyike ili umma utambue ukweli wa sakata hili. Yeye mwenyewe pia amekanusha na yuko tayari kutoa ushirikano ili ukweli ujulikane. Baada ya kufuatilia kwa karibu nimejiridhisha kuwa huyu bwana mdogo hajakula mlungula na naamini kuwa wanaosambaza hujma hizi ni sehemu ya mafisadi, wanajua huyo ni mwiba kwao. Na pia naona kuna missunderstanding kati ya Zitto na waziri.

    Mpenda maendeleo.

    ReplyDelete
  10. Bwa Zitto naona unatumia nguvu nyingi kujieleza hata kama umelamba shida ipo wapi so long hawana ushahidi hilo usihofu ila uelewe when you want to go high you should expect no body is happy hivyo lazima utafutiwe zengwe la kukubebesha. Nakukumbusha tu najua siasa umeanza mdogo sana ukiwa na kadegree kamoja kumbuka bro Sallim Ahmed Sallim just two or three weeks ya uchaguzi akavishwa joka la shingo kuwa yeye ni Hizbulla pamoja na u Dr wake hakuelewa kwa nini kavishwa taji la joka la Uhizbulla wacha ahangaike nalo kujivua oooh mimi sio hizbulla oooh jamani hivi na vile kasahau kabisa kutafuta kura watu haoooooooo sasa wewe acha kupoteza muda mwingi umelamba hukulamba wao ndio wape kazii ya kuprove beyond resonable doubt kwamba umelamba otherwise tunajua kuwa hizo ni njia za kukuchafulia nafasi ya urais achana nao endelea na strategy zako za urais.ila pole kijana wangu joka la shingo unalo

    ReplyDelete
  11. Hata wakuseme nini wewe kwangu ni safi tu. Chadema siipendi kabisaaa lakini wakikuteua kugombea urais nitakuchagua, kijana safi mchapa kazi unaependa walalahoi na posho hupokei wanakuonea wivu. Mungu atakunusuru kama umechukua hujachukua wewe safi nani kama wewe asimame mungu amuangushe. Big up NYEPESI.

    ReplyDelete
  12. sitajisumbua kuchangia tena unanibania sana kwani umekuwa chadema au unawaogopa. ziti hana matatizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...