Mkulima wa zao la tangawizi kutoka kijiji cha madaba songea vijijini Pascal Minambi kulia akimuonesha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aina ya tangawizi inayolimwa katika kijiji hicho,wakati wa maonesho ya kilimo maarufu nane nane mkoani Ruvuma.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kulia akiangalia moja ya trekta kutoka kikosi cha jeshi la kujenga taifa mlale jkt wakati wa maonesho ya nane nane mjini songea.
Mtaalamu wa zao la Tumbaku mkoani Ruvuma Benedict Tembo akimuonesha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kulia, tumbaku iliyokaushwa kwa moshi inayolizalishwa katika wilaya ya Namtumbo mkoani humo wakati wa maonesho ya wakulima nane nane mkoani Ruvuma kulia kwa mkuu wa mkoa ni mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti.
Mtaalamu wa dawa za asili ambaye hakufahamika jina lake kushoto akimuonesha dawa za asili mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kulia, wakati wa maonesho ya wakulima nane nane mkoani humo yaliyofanyika katika kata ya msamala manispaa ya Songea.
Akiangalia makopo ya kahawa inayolimwa wilayani mbinga wakati wa maonesho ya wakulima maarufu nane nane.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiangalia viazi vikuu katika moja ya mabanda ya maonesho ya wakulima mjini songea kulia mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti.
Mfanyabiashara wa dawa za kilimo aliyefahamika kwa jina moja la Makamba kulia,akiomuonesha mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aina ya mbegu ya kisasa ya ufuta iliyoanza kuzalishwa mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wa nne kushoto akiangalia kitalu cha maharage ya kisasa katika maonesho ya wakulima maarufu nane nane mjini songea. PICHA NA MUHIDIN AMRI










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...