Mtoto ameokotwa eneo la PPF Tower, Jijini Dar Es Salaam saa sita mchana wa leo. Amekutwa amelala chini eneo hilo.

Ameletwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Askari wa Central Police. Mtoto huyu anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu hivi, kwa hiyo hawezi kuongea.

Yeyote anayemfahamu mtoto huyu au wazazi wa mtoto huyu ajitokeze na kutoa taarifa sahihi kwetu kupitia namba yangu 0755 64 86 36 au 0715 64 86 36.

Mtoto tunaye Hospitalini, anaendelea kuhudumiwa. Tafadhali sambaza barua pepe hii.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Huyo mzazi wake akipatikana achapwe viboko hayuko serious!

    ReplyDelete
  2. Nani kamtupa tena huyu mchumba mzuri hivi?

    Wahusika wasipopatikana tunaomba tangazo jingine tuje kumchukua huyo mtoto.

    David V

    ReplyDelete
  3. Ni jambo jema lililofanyika kumuokota mtoto huyu na kumpeleka hospital wakati mawasiliano ya kuwatafuta ndugu na jamaa yakiendelea. Nina swali lakini, huyu mtoto ana sifa gani za kuokotwa na kupelekwa hospital na kutafuta ndugu zake, ukilinganisha na wale ambao tunawaona wegi tu mtaani wamelala. Au tunaagalia mtoto wa kuokota ni yule aliyevaa nguo za dukani??? Tuwe na tabia basi ya kuwaokota watoto wote mtaani na kuwapeleka hosptal kama wanaumwa na hatua za kutafuta ndugu zao zifanyike kama ilivyofanyika kwa huyu.

    ReplyDelete
  4. kwani mtoto huyo anaumwa mpa kapelekwa huko hospital?inaonekana mama yake wamepoteana,,maana hawezi mtu kumtelekeza mtoto wakati kamlea mpaka kufikia hapo,,na kamvalisha vizuri tu Ma'ansha'Allah
    Ahlam,london

    ReplyDelete
  5. What a beautiful child,hope all ends well

    ReplyDelete
  6. Hivi jamani , aliyetoa comment za mama wa mtoto akipatikana achapwe viboko,anakaa nchi gani ???? isiwe kule kule !! huyu mama hajakosea kitu, bali mtoto kaambaa ambaa mwenyewe mpaka akampoteza mama yake-na huyu mama huko aliko lazima anahangaika kumpata mtoto wake. Namsifu sana aliyesema kwamba ,VIPI hao watoto wengine wanao-onekana mitaani na nguo chafu na bila viatu, je ?? nao tuwaokote ?? Kumbe kitu matunzo,ha !! Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  7. Sasa na nyie huko Muhimbili, vipi hiyo picha ??? , mmemfinya kwanza mpaka akalia ili picha ionekane kutia huruma au ?? hii ni mitindo ya world vission-wanaotangaza michango ya kusaidia watoto africa,maana picha zao zote ni za watoto aidha wanalia au wachafu na wamejaa inzi-huyu kavaa vizuri namna hii kamwe hawamuweki kwenye TV. Wanaaibisha Africa. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  8. zebedayo nenda kajibu ile hoja ya TRA na CT SCAN ulizoikacha kule juu, yaelekea we ni muoga wa changamoto nzito ingawa unajua zaidi kuongea pumba kwenye mada nyeti ila we nenda tu, tuone mawazo yako.

    ReplyDelete
  9. zebedayo umenichekesha na umesema kweli. hivi walikuwa na haraka gani hata wasisubiri mtoto anyamaze? kuna ile charity ya oxfam, jamani picha zake zinanikera.

    ReplyDelete
  10. Mtoto hakutendewa haki kabisa!

    Amedhalilishwa sana,

    Amekwazwa sana na ameathiriwa mno Kisaikolojia!

    Na sasa hana jinsi analia!,

    Hivi mtoto akue akiwa mkubwa aje aonyeshwe picha hii akiwa mdogo analia baada ya kutelekezwa na wazazi/ walezi atafurahi?

    Kwenye Mchakato wa Katiba tuingize muswaada wa kuwabana wanaofanya ulezi wa kizembe namna hii!

    ReplyDelete
  11. Ni wakati muafaka wa Kuijenga Jamii ya Tanzania kwa Sera ya malezi Shirikishi baada ya kupata mafanikio ya Polisi shirikishi /Polisi Jamii.

    Maisha yetu ktk jamii yetu nchini yana mgawanyiko kulinga na majaaliwa kama hapa:

    1.Wapo wazazi wanaotafuta watoto hawakupata Majaaliwa.

    2.Wapo waliojaaliwa uzazi lakini hawawataki watoto, au hawana uwezo wa kutoa matunzo ya malezi.

    Je, kama zinavyofanya Misheni za Kidini kwa nini Serikali zetu za Mitaa zisifanye mchakato wa kuwaunganisha wenye mahitaji ya watoto baada ya wenye watoto kuona hawana uwezo wa malezi?

    Kwa nini watu wafikie hatua za kutelekeza watoto badala ya kuwakabidhi kwa busara na utaratibu watoto ktk Vituo Maalum vya Mamlaka?

    Pamoja malezi shirikishi inawezekana Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...