Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ahsante sana Mhe. Raisi JK kwa Uongozi wa kivitendo.

    Waeleze Mafisadi,Wezi na Wala rushwa ya kuwa uhujumu sio akili,ubunifu, ujanja, kigezo cha mafanikio, au muamko wa maendeleo ni kuwa hata kupitia Kilimo maisha yanawezekana!

    ReplyDelete
  2. Sawa, Raisi Jakaya Kikwete kwa kushiriki kilimo kama njia ya kumudu maisha na ajio matarajio ya baadae.

    Pana mtazamo wa baadhi ya watu miongoni mwa jamii yetu wanachukulia kuwa wizi,ufisadi na uhujumu ndio akili ya kutafuta maisha na sio uovu!

    ReplyDelete
  3. NIMEPENDA DIRAA . tUVAE WOTE KAMA WASOMALI. vAZI ZURI HILO

    ReplyDelete
  4. Mfundishe na Ridhiwani hii kazi inamfaa sana

    ReplyDelete
  5. I love this president for his simplicity, he takes easy for everything, no complecations at all.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Tano hapo juu Anoinymous wa Thu Aug 23 02:56:00 AM 2012

    Kweli Ridhiwani anafaa sana kuwa Mkulima kwa kilimo kwa sifa hizi hapa chini:

    1-Ni kijana na msomi.
    2-Ni mchapa kazi na mwepesi.
    3-Atashawishi wengi ktk jamii kushiriki kilimo.

    ReplyDelete
  7. Ridhiwani kushiriki Kilimo itakuwa ni kigezo chama, kama mama yake Mama Salma Kikwete ni FIRST LADY, hivyo Ridhiwani atakuwa ni kigezo chema kwa kuwa FIRST SON nchini!

    ReplyDelete
  8. Mhe Rais umetenda vyema utaalam huo uenee kwa wanakijiji wenzako na hata TZ kwa ujumla. Hongera sana.Ernest

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...