Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Yusuph Mwenda wakati akiwasili kwenye msikiti wa Kinondoni kwa ajili kujumuina na waislam wengine kwenye swala ya Idd el Fitr,mapema leo asubuhi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Masheikh kabla ya swala ya Idd el Fitr mapema leo asubuhi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa miongoni wa waumini kusikiliza mawaidha kutoka kwa Sheikh Abubakar Zubeir katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam baada ya ya Swala ya Idd leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipena mkono wa Idd el Fitr na waumini wenzake wa kiislam baada ya swala hiyo ya Idd el Fitr,katika msikiti wa Kinondoni,jijini Dar es Salaam leo.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akipeana mkono wa Idd na waislam wenzake mara baada ya swala ya Idd el Fitr katika msikiti wa Kinondoni,jijini Dar es Salaam leo.PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. yule mwanajeshi anaekaa nyuma ya kikwete leo ameenda likizo?simuoni

    ReplyDelete
  2. Yupo hujamwona?? Mwangalie vizuri kapiga kanzu na kofia , yupo nyuma ya Mh anapiga kazi Kama kawaida sema kanzu na barakaShea vimbadilisha

    ReplyDelete
  3. Mzee unaonekana humjui huyo mwanajeshi unayemsema, hivi kweli humwoni yuko hapo nyuma ya kikwete amevaa kanzu na barakashea kama kikwete, mwangalie hapo kikwete anaposhuka kwenye gari yuko nyuma yake na hiyo picha ya pili yuko nyuma yake, inaonekana wewe unamtambua kwa mavazi ya kijeshi akibadili humfahamu.
    Pole sana, mzee wa kukariri.

    ReplyDelete
  4. Humu yukoktk amani hakuna wasiwasi juu ya usalama wake.

    ReplyDelete
  5. noamba kuliza , huyu mwanajeshi nasikia jina lake ni John, sasa John inaendana na Kanzu ?? samahani lakini.

    ReplyDelete
  6. Mbona waarabu wakristo wanavaa kanzu? Kanzu ni vazi tu siyo dini.

    Na wale mapadri na wachungaji wanovaa kanzu au kwa kuwa zimenakshiwa unadhani ni tafauti?

    ReplyDelete
  7. nimerudi tena, hapa mmeweka picha ya wanawake kwa vile first lady alikuwepo, vinginevyo mngewabania kama kawaida yenu, hivi nyie wanaume mmepikiwa futari weee halafu mnajioona nyie ndo watu peke yenu, next idd tunataka usawa humu ndani, kama vipi michu hamna kurusha picha za wanaume peke yao, kwani si wote walifunga na kwenda misikitini, iweje inatoka jinsia moja tuu? tunataka haki sawa humu ndani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...