Mmoja wa Wazee wa Iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bibi Nazarine Mwagala akifanya maombi muda mfupi kabla ya kufungua mkutano wa wazee wa jumuiya hiyo ambao hukutana kila siku ya Alhamisi kupeana taarifa za maendeleo ya kesi yao ambayo wameifungua kwenye Mahakama ya Afrika kanda ya Arusha ambapo kwa mujibu wa maendeleo ya kesi hiyo kuna kila dalilili ya kupata ushindi.
Nuru Hamisi nae alisoma dua kwa niaba ya Waisilamu kwenye Mkutano huo.
 Hapa Wazee hao wakinunua dokument za mwenendo wa kesi hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango kwaajili ya kulipia gharama mbalimbali za kuendesha vikao hivyo.
Wazee hao wakiwa wamechanganyika na vijana ambao ni warithi wa deni hilo waliloachiwa na wazazi wao wakifuatilia kwa makini mchakato wa kesi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Eti Wazee wananunua dokumenti kufuatilia mwenendo wa kesi! Hivi hamchoki kuwakamua hao wazee wetu? Au mpaka muone matone ya damu yanawatoka ndio mjue jinsi mnavyodhulumu wanyonge?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...