AJALI nyingi za barabarani nchini husababishwa na madereva wazembe wasio zingatia sheria za matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa ajali hizo nyingi husababishwa na madereva hao kuovatake magari mengine katika kona au milima kama basi hili linavyofanya katika kona ya Lugalo mkoani Iringa. Madereva “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
Basi hili linguine nalo lilikuwa linafanya makopsa hay ohayo ya kulipita gari linguine katika miinuka na kona kali za mlima Kitonga.
 
Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Iringa, akiwepo RTO, SP. Pamphil Honono (kushoto) walimuona na kumsimamisha dereva wa basi hilo. Matukio haya yanatokea ndani ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. 
  
Nahapa Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani akimwandikia Notfication dereva huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nafikiri kwa hili mmeingilia privacy ya huyu dreva, kuweka leseni yake na taarifa zake hadharani hivi sio sawa. Au wazee nyie hamjui mambo ya identity thefy?

    ReplyDelete
  2. Hongera sana, ulie tutumia kisa hiki, Madereva kuweni makini, si huko njia za mikoani hata humu humu ndani ya miji, wengi wamekuwa na haraka zisizo na sababu, hawajui kuwa kuto kusubiri kwa dakika moja tu kunaweza kuleta madhara makubwa kwa dereva na raia wengine na mali zao. Mdau Sixmund

    ReplyDelete
  3. nampa hongera mtoa taarifa. ila napenda kusema kuwa mimi niliwahi kumpatia taarifa traffic katika njia ya dar segera- na swala hilo nililiandika hapa. chakusikitisha hatukuona mwitikio wowote wa viongozi traffic. nasikitaka kusema sio muda mrefu basi hilo lilileta ajali. swala sio kuwapa noticefication.. hiyo ni kitu kidogo. nafikiri kwa ushahidi kama huu dereva angefungiwa na pia kuondolewa katika passenger's driver. pili pia ingekuwa yanatolewa matangazo hayo ikaonekana kuwa hatua zinachukuliwa. wenzetu ndio wamefikia hayo kwa kuwa strict.
    mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...