Shirika la Turkey’s Kuveyt Turk investment lina mpango wa kufangua benki ya kwanza inayofuata sheria za kiislam nchini Ujerumani. Shirika hilo lina mpango wa kufanya hivyo mwezi wa kumi mwaka huu 2012 kwa matumaini kwamba athari mbaya zinazotokana na uchumi wa nchi za ulaya, zinaweza kupunguzwa  na benki hizo ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa.

Muasisi na mkurugenzi wa Institute for Islamic Banking and Finance (IFIBAF) ndugu Zaid el- Mogaaddedi aliopo ktk mji wa Frankfurt nchini Ujerumani, alinukuliwa akisema ‘fikra nzima ya benki zinazofuata sheria za kiIslam ni kufuata maelekezo na kanuni za kiIslam.

Benki zinazofuata sheria za kiIslam zimeanzishwa nchi mbalimbali ktk bara la ulaya lakini wataalamu wa kiuchumi wamekadiria kwamba benki hiyo inaweza kufanikiwa sana nchini Ujerumani kuliko ilivyofanikiwa nchini Ufaransa na uingereza. Changamoto kubwa ni ile inayohusiana na uwezo wa benki za kiIslam kua na miundombinu na huduma nzuri alisema  El-Mogaddedi.

Ujerumani ina idadi ya Waislam milioni 3, 8 hadi 4,3 ambao ni sawa na asilimia tano ukilinganisha na idadi ya wakazi wa Ujerumani ambao idadi yao ni milioni 82. Benki hiyo inawalenga waislam na wasiokua waislam. Uchumi unaofuata sheria za kiIslamu ni ktk moja ya uchumi ambao unakua kwa haraka sana duniani. Ktk jumla ya sababu za kukua kwa uchumi huo, ni pamoja na Waarabu kuondoa pesa zao nchini marekani na kuziweka ktk nchi za kiIslam ikiwemo Malysia na bara Arabu, baada ya uvamizi maarufu unaojulikana kama 9/11, ikifuatiwa na uchumi huo kuingiza faida ktk kipindi ambacho uchumi wa dunia ulitetereka. Kwa maelezo zaidi kuhusu uchumi na benki zinazofuata sheria za kiIslamu tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni hatua nzuri kwa ujerumani kuzikaribisha benki hizo na kujaribu kuzifahamu zinafanya kazi vipi. kiukweli kabisa mipangilio ya kiuchumi duniani mingi inakosa maadili

    ReplyDelete
  2. Hii habari ni nzuri na inafahamisha jambor muhimu la ufanisi wa kiuchumi kupitia mfumo ambao hata nchi zilizoendelea zimeona ndiyo mkombozi wa kuteteruka kwa uchumi wao. Sisi ambao uchumi wetu uko chini tunauhitaji zaidi mfumo huu. Je tunasubiri niñi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...