Ndugu wanahabari,
Karibuni katika mkutano mfupi ambao unalenga kuzungumzia ama
kuelezea masikitiko makubwa dhidi ya Kocha wa Timu ya Yanga TOM SAINTFIET (pichani) aliyoyatoa kwa vyombo vya habari kuidhalilisha
hoteli yangu juu ya huduma zake na kiwango chake
alichokiita cha huduma mbovu!.
Kimsingi management ya Peter safari’s Hotel na Uongozi wa
chama cha wamiliki wa Mahotel Mkoa wa Mbeya, tumesoma na kusikiliza kwa
masikitiko makubwa lawama zilizotolewa na Kocha huyo kuwa “hajawahi kulala
kwenye hoteli ya hadhi ya chini kama hii katika nchi 20 alizowahi
kufanya kazi katika nchi za Afrika”.
Uongozi wa hotel na chama cha wamiliki wa hotel kwa ujumla
kinachukulia suala hili kama kampeni maalumu ya kudhalilisha na kukatisha tamaa
wateja kuiona mbeya haina hotel za hadhi za kuishi timu na watu wenye hadhi
katika jamii, kitu ambacho si kweli na ni visingizio kutokana kushindwa kwake
kuwezesha timu kufikia matarajio ya mashabiki na wapenzi wa timu
hiyo.
Kimsingi viongozi wa Timu ya yanga waliomba kuwalaza wachezaji wawili
katika kitanda kimoja tofauti na taratibu za hotel na hii ilitokana na
mipangilio yao hasa kwenye suala la uwezo wa kulipia kila mchezaji chumba
chake, aidha, uongozi wa hotel ulijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha
kuwa wachezaji wanapata huduma walizohitaji na hata wakati mwingine kutoa usafiri
kwaajili ya kununua mahitaji ya familia zao kitu ambacho hakifanyiki maeneo
mengine kwa gharama za hotel.
Kwa kutambua madhara yaliyotokana na matamshi ya kocha huyo raia wa
Ubelgiji, Uongozi wa hotel ya Peter Safaris unayaona matamshi haya
kama udhalilishaji mkubwa na wenye nia mbaya ya kuuharibia mkoa wa
mbeya na kuutangaza vibaya kwa wageni juu ya uwezo wake
katika utoaji wa huduma za hoteli.
Aidha kwakuwa maneno ya kocha huyo yametamkwa na
kutangazwa kwenye vyombo vya habari pasipo kukanushwa na viongozi wa Timu ya
Yanga ambao ndiyo waliofanya maandalizi na kufanya mazungumzo ya
maombi ya kuwalaza wachezaji wawili katika vyumba ambavyo vina uwezo
wa kulaza mtu mmoja (single), Peter safaris inaliona jambo hilo kama ni sehemu
ya kashfa iliyojengwa kwa nia ya kuiharibia hotel biashara na
kuipotezea hadhi mbele ya wageni na watumiaji wa huduma za PETER
SAFARIS ambayo inaendelea kupanua huduma zake kwa mkoa wa mbeya na
maeneo mengine.
Ikumbukwe kuwa Peter safaris hotels imekuwa ikipokea wageni wa hadhi
mbalimbali wakiwemo viongozi wa ngazi za kitaifa, wageni kutoka nje wa hadhi za
juu na wafanyabiashara wakubwa, hivyo ugeni wa Yanga na hadhi inayozungumzwa na
Kocha huyo hauwezi kufikia mahala pa kuidhalilisha hotel kwa kiwango hicho
ambacho kocha huyo amevitumia vyombo vya habari licha ya hotel kutopata maoni
yoyote baada ya timu kuhudumiwa kwenye sanduku la
maoni(suggestion box).
Kutokana na hali hii iliyojitokeza, uongozi wa Hotel unautaka uongozi wa
Yanga kuiomba radhi management ya Hotel ya Peter safaris kwa lugha ya kashfa na
isiyoendana na utamaduni wa Mtanzania kwakuzingatia kuwa wachezaji wakiulizwa
namna walivyohudumiwa wasingeweza kuzungumza hayo ambayo mwalimu wao
ameyazungumza kwa utashi wake.
PETER SAFAR’s inalichukulia jambo hili kwa uzito unaostahili
kwakuzingatia kuwa lugha iliyotolewa na mteja wake huyo imevuka
kiwango cha kuvumilika, na njia pekee ambayo tunadhani ni ya uungwana kabla ya
kuingia kwenye taratibu za kisheria ni kuwataka YANGA kuomba radhi kwa lugha ya
dharau na kashfa dhidi ya hotel yetu vinginevyo tunakusudia kuchua hatua za
kisheria kwa kuzingatia kuwa hotel inaendeleshwa kwa mujibu wa taratibu na
sheria zinazotawala huduma za hotel na zile za mipango miji ambazo
masuala ya usafi ni miongoni mwa maeneo muhimu ya kukidhi viwango vya
uendeshaji wake.
Nawasilisha
MKURUGENZI MTENDAJI
PETER SAFARI’s HOTEL
MBEYA.
weka picha ya hiyo hoteli tuone. weka vyuma, toilets, restaurants na menu zenu... sisi ndio tuamue
ReplyDeleteSasa kama ni kweli asiseme?
ReplyDeleteDuu wachezaji wawili tena wanaume kitanda kimoja, ndiyo maanda Yanga hawakushinda..... Kimaadili ya kitanzania hotel iliruhusu vipi watu wawili wa njisia mmoja kulala kitanda kimoja? au hotel Peter Safari's hamna wateja tokana na huduma nzenu mbaya ndiyo mukawarundika wachezaji wa Yanga?
ReplyDeleteama hakika mie naungana na uongozi wa hoteli hiyo kwa kukanusha vikali uongo huo wa kocha huyo. Hoteli hiyo ni nzuri, na ina huduma zote muhimu ambazo mtu wa hadhi ya wachezaji wa Yanga anastahili kuzipata. Mie mwenyewe nilikuwa na wageni wangu wa hadhi ya standard, ambao walifikia pale kwa muda wa wiki tatu, nisisikie malalamiko yoyote toka kwao, maana kama kungekuwa na mapungufu, lazima wangetaka niwahamishie pengine. Isitoshe, walirudi siku nyingine na kukaa palepale.
ReplyDeleteHuyu bwana wa kizungu anataka hoteli ya hadhi gani?Nyota tano? Hatuna hoteli hiyo huku Mbeya, lakini tuna hoteli ambazo zinaweza kutunza watu wa standard ya juu, wakaishi comfortably.
Huyu kocha asitake kuleta visingizio vya kipuuzi, ili ku-justify kushindwa kwake kuifunga Prisons
-Embe Kidusu
NI WAZI KABISA HIYO HOTEL INAENDESHWA SI KWA MISINGI YA KIBIASHARA, CRITIQUES KUTOKA KWA WATEJA NDIO CHANGAMOTO ZA KUBORESHA HUDUMA ZENU. MSICHUKULIE COMMENTS MSIZOZIPEDA KUWA NI KUBOMOA BIASHARA. BADILIKENI KUBALINI KUKOSOLEWA ILI KUONGEZA UBORA WA HUDUMA KWA WATEJA.
ReplyDeleteHotel inayofuata taratibu na sheria hailazi watu wawili kwenye single room, huo ndo udahifu wenu wa kwanza. Mgekataa biashara na yanga kama kweli mnafuata sheria lakini kitendo cha kulaza watu wawili room ya mtu mmoja inaonyesha pia ni likely mkaenda kinyume na standard za huduma.
ReplyDeletesasa kwa nini mlishusha standard zenu kwa kukubali kuweka watu wawili? that is the cost!!swallow it!!
ReplyDeleteInteresting.
ReplyDeletewengine hapa hatujui alichokisema huyo kocha ninini, lakini ni wazi ana huyo kocha ana exposure kwa hiyo kuna nafasi kubwa ya kumuamini kuliko mkurugenzi mtendaji wa Peters safari hotel ambaye tunamjua tu kwa maandishi yake hapo ambayo msomoje yeyote makini ataona kwamba yuko defensive so hana credibility, for example ana defend hoteli lakini anaongelea lugha iliyotumika haiendani na utamaduni wa kitanzania? wewe ni mfanyabiashara kama wateja hawajaridhika lazima waseme. Tafuta hotel inspector BBC uone wamiliki wa hoteli wenzio wanavyopigwa vijembe wazi wazi and they learn.
Badala ya kuomba kuobwa radhi nafikili mngemuomba huyo bwana awaeleze ninini alitegemea kupata kizuri ambacho hakikuwepo, basi mnajifunza kutoka hapo kama anaongea pumba mnamwambia.
culture za kitanzania za
kuambiana kwa kumbelezana inabidi ziishe kikolo, imbombo kamagi.
Huyu bwana Embe Kidusu hapo juu nahisi si mtu wa kiwango na nahisi hata wageni wake si wa kiwango cha kuchukulia mfano. Kama hiyo hoteli ingekuwa ya hali ya kiwango kinachokubalika, basi isingeruhusu watu wawili wa jinsia moja walale kitanda kimoja. Kwa kukubali tu ina maana ni hoteli ya kiwango duni. Hata hao wageni wako ni wa kiwango cha kulazwa wawili katika kitanda kimoja ndio maana hawakulalamika. Kwani ukileta mtu aliyezoea kulala katika tembe unadhani atalalamika. Angalia hadhi ya wageni wako ndio uwafanye kama reference
ReplyDeleteKuna mameno mitaani kwamba kocha hakuoga hadi anakwenda kwenye gemu!!! Je, hii nayo ni kweli? Je, chumba alicholala kocha kina hadhi ya kimataifa?
ReplyDeleteKuna mameno mitaani kwamba kocha hakuoga hadi anakwenda kwenye gemu! Je, hii nayo ni kweli? Je, chumba alicholala kocha kina hadhi ya kimataifa?
ReplyDeletehampendi kuambiwa ukweli, hata mimi nilishalala hapo huduma si za kuridhisha kwa kweli, wabongo tumezoea kusifiwa tu, badilikeni non sense , kama mtu hakuridhika asiseme? ilikuwa inabidi mumumulize wapi mlipokosea , sasa nyie mnakuja juu, na tena ndio mzungu ndio kabisaaaaaa mnatumia muda kusema mnazalilishwa loh. Aibu toeni hapa malalamiko yenu, mkaongee naye mwenyewe, aombe radhi aibu aibu loh. Customer Service zero inavyoonekana, ingekuwa nzuri msingekuja kuweka humu grow up, business ni ushindani. Mteja ni mfalme
ReplyDeleteMmejishitaki wenyewe kwa kuvunja sheria na kuwalaza watu mzungu wa-nne. Sasa Polisi watawabebena kama senene, kila siku ka-elfu hamsini na ushehe ili mambo yasifike mbali.
ReplyDeleteA customer is always right. The only way to prove critics wrong is to transform their negative views into positive by improving services when necessary. Also it is completely unprofessional to assign two unrelated adults a single hotel room. It may be legal in your jurisdiction, but it sounds weird in civilized world. Please feel free to fact-check my comments with other hotel professionals worldwide and try to get better.
ReplyDeleteHii mikwara ya kushitakiana walianza watu wa siasa na sasa imeingia kwa huyu jamaa.
ReplyDeleteMtu mwenye kushitaki kweli haongei na vyombo vya habari, anachukua hatua.
Ignorant
WENYE HOTELI ACHENI USHAMBA. MNALETA PROPAGANDA ZA KISIASA ILI MTETEE HOTELI YENU WATEJA WASIKIMBIE. TUMESHAJUA KUWA HOTELI YENU IMECHOKA NI HOTELI UCHWARA IBORESHENI.
ReplyDeleteMSILAUMU KOCHA WALA UONGOZI WA YANGA NYIE NDIO WAROHO WA PESA, KAMA MLIONA VYUMBA HAITOSHI MNGEKATAA KUWA NAFASI HAITOSHI.
MNAPENDA SIFA WAKATI PERFORMANCE NI SIFURI. KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA KAMWE HAMTABORESHA HOTELI YENU MAANA HAMKUBALI MAPUNGUFU YENU. UJINGA MTUPU.
SIE WENGINE TULIKUWA HATUJI KINACHOENDELEA ILA UBISHI WENU NA MANAZIDI KUJIHARIBIA. ENDELEENI TU NA KUTANGAZA UOZO WENU MTAONA WATEJA WATAKAVYOPUNGUA
ETI MNAJITETEA MLITOA HADI USAFIRI WA KUWAPELEKA WACHEZAJI SOKONI KUNUNUA MAHITAJI YA FAMILIA ZAO. KWA HIYO HICHO NDIO KIPIMO SAHIHI CHA UBORA WA HOTELI?
HOJA AU POINTI PEKEE INAYOONEKANA HAPO NA AMBAYO WANAITUMIA KUTETEA HOTELI YAO NI USAFILI WA WACHEZAJI KWENDA SOKINI BASI. HAKUNA JINGINE.
ReplyDeleteHII INAONYESHA JINSI GANI WATU WANATAKA SIFA KWA LAZIMA.
UKILALA HIYO HOTELI INABIDI USIFIE TU HAKUNA KUKOSOA.
Mimi nafikiri imefika wakati kwa watanzania hasa wafanyabiashara kutambua umuhimu wa MTEJA. Na kwamba HAKUNA MTEJA MZURI kushinda MTEJA ALIYE TAYARI KUKUKOSOA. Tuache tabia ya KUJITETEA pasipo MSINGI wowote. Katika karne hii, ni muhimu biashara zikawakumbatia wakosoaji maana WANATUTAKIA MEMA. Tusiwe wale watu tunaojali faida za muda mfupi kwa kigezo cha kuogopa kuchafuliwa..eti tunaaribiwa biashara...TUKUMBUKE KUWA NI WATEJA WACHACHE SANA walio tayari KUTOA MAONI BILA UNAFIKI. JAMBO LINGINE LA MSINGI SANA..KWA NINI MNATABIA YA KUPINDISHA SERA/POLICY ZENU? Kwa kifupi KITENDO CHENU CHA KURUHUSU WACHEZAJI KULALA WAWILI NDICHO KINAWAONGEZEA KASHFA. UONGOZI LAWAMA NI ZENU na KATU MTEJA HALAUMIWI; SIKILIZENI ALICHOWAAMBIA MTEJA..REKEBISHENI KWA MANUFAA ya HOTELI YENU na WAKAZI wa MBEYA...AIBU SANA
ReplyDelete
ReplyDelete1. Mteja ni mfalme
2. Usafiri wa bure kwenda na kurudi "mall" hiyo ni standard kwenye hoteli yoyote ya ' kimataifa.
3. Nyinyi wenyewe ndio aw kulaumiwa kwa kukubali ku check in midume miwili on same room same bed!!!
4. KAMA HOTELI LAZIMA MKUBALI KUKOSOLEWA NA NDIO MAANA KUNA "SUGGESTION BOXES" yaani masanduku ya maoni.
Huyo mtu ni lazima amekwishakaa kwenye mahoteli tofauti ndio maana amefikia kusema hivyo.
Hili ndio tatizo letu Watanzania, pale mtu mwenye uelewa na upeo peke anapotoa comments kuhusu mapungufu/ubovu wa kitu fulani huwa anaonekana ni mtu adui!
ReplyDeleteMimi ningefurahishwa na uongozi wa mahoteli mjini Mbeya kama ungeliyafanyia kazi maelezo yaliyotewa na bwana Saintfiet kwa kuboresha huduma katika mahoteli yao na si kusema kwamba aliyoyasema si sahihi!
Mimi mwenyewe msafiri karibu katika mikoa yote hapa Tanzania, lakini kuna baadhi ya mikoa tena mingi tu ikiwa ni pamoja na Mbeya huwa naboreka sana na huduma zao za kihoteli, sembuse mtu kutoka bara Ulaya?!
....tubadilike jamani!!!
Hotel hii kweli si ya hadhi na maneno aliyosema kocha ni ya kweli. Tanzania customer service ni sifuri huduma mbovu mkiambiwa mnaanza kukanusha kama hivi. Biashara inatakiwa uchukue hii changamoto na kuirekebisha sio kuanza mambo ya siasa ya propagana.
ReplyDelete