Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma,Muhidin Gulumo (kushoto) akiimba sambamba na Hassani Moshi 'Tx Jr' wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam usiku huu.Gulumo ni mwanamziki Mkongwe pekee aliyedumu katika Jukwaa kwa mda mrefu hapa nchini ambapo hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na Maradhi lakini kwa sasa karudi ulingoni kukonga mashabiki wa bendi hiyo.msondo kila jumapili inatumbuiza katika ukumbi wa Max Bar.
Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani wakati walipokuwa wakitumbuiza katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam usiku huu,kutoka kushoto ni Muhidini Gulumo,Hassani Moshi na Shabani Dede.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ndiyo Baba ya Muziki,Msondo Ngoma Music band,ni bendi pekee kongwe barani Africa,Msondo ilianza 1964 (Nuta Jazz).
    Wadau
    FFU Ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Ndiyo Baba ya Muziki,Msondo Ngoma Music band,ni bendi pekee kongwe barani Africa,Msondo ilianza 1964 (Nuta Jazz).
    Wadau
    FFU Ughaibuni

    ReplyDelete
  3. Huyu mzee pamoja na umri wake lakini sauti yake ni ile ile ya mwaka 1974. Kwa kweli nafurahia sauti yake kwenye nyimbo alizoimba tangu Sikinde na sasa Msondo. Mungu akupe afya njema uendelee kutupa burudani!!

    ReplyDelete
  4. yes imeanza mwaka 1964,angalia vyombo chakavu ile mbaya,bado wana mic za kamba ,stendi zimejaa kutu.Nyie FFU mmeanza juzi juzi tu,vifaa vyenu vya kileo. Je ? kuna sababu . Au labda kazi ilikuwa baada ya muziki wanaishia guest kuosha jando,matokeo ndo hayo from 1964.

    ReplyDelete
  5. Pole sana Mkuu, nakukumbuka kwa nyimbo nyingi sana ulizoimba na Sikinde pamoja na Msondo kama vile;Selina,Kasimu,Ford,Mjomba,Usimchezee Chatu,Nitakaza roho,ukitaka kufurahi kila j'mosi...... nk

    ReplyDelete
  6. Hili NUNDA la 04.55 limetoka wapi? mbona linaandika utumbo badala ya kuwapa dole? 2@$%^&* mkubwa

    ReplyDelete
  7. maalim tafuta msala umalizie umri wako kwa kumcha Mola wako.ulipopata panatosha

    ReplyDelete
  8. MADAU WA 7 HAPO JUU Anonymous wa Mon Sep 10, 10:55:00 PM 2012

    Naungana na wewe kwa kauli yako ya kuwa sasa ni wakati wake kugeuza ukurasa kwa alichokipata na aongezee kwa kutafuta msala na tasubihi ili kupata faida zaidi!

    Inshallah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...