Wachezaji wa michezo ya aina mbalimbali ya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakipita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi
 Kikosi cha timu ya Ikulu, mchezo wa mpira wa netiboli , wakijpanga kabla ya kuanza mchezo
 Kocha Hellen Siboka (kulia) akiwa na kikosi chake kabambe cha timu ya Ikulu kabla ya kuanza mchezo
 Kikosi cha timu ya mpira wa Netiboli Ofisi ya RAS Kilimanjaro , wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukosa mshindani
Baadhi ya wachezaji na viongozi wa timu ya Netiboli ya Ukaguzi wakitoa uwanjani baada ya sare ya bao 27-27 dhidi ya Uchukuzi
Hapa ni patashika kati ya timu ya Netiboli Wizara ya Kilimo (jezi za mchezaji aliyeshika mpira0  VS timu ya Maji leo ambapo  Kilimo ilishinda bao 32- 22.
Timu ya mpira wa Netiboli ya Ikulu, ikikaguliwa na Mwamuzi , baada ya kumaliza kuikagua timu ya Tume ya Utumishi.


Picha zote na habari John Nditi, 

wa Globu ya Jamii, Morogoro

WAZIRI wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Dk Finella Mukangara, amezitaka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zihakikishe zina kuwa na bajeti ya kutosha ya michezo ili kutafsiri dhana zima ya Serilali
ya kupenda na kuhimiza michezo kazini. Pia amesema  ni wajibu wa kila Wizara, Idara na Taasisi za Serikali ,Vyama vya Michezo na sehemu za jamii kuwajibika kimatendo  katika kukuza na kuendeleza michezo.

Dk Mukangara alisema hayo  Septemba  22, mwaka huu katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mashindano ya  32 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali ( SHIMIWI)  kwa mwaka 2012 yanayofanyika Mkoani Morogoro na kuwashirikisha  zaidi ya  wanamichezo 3,000 kutoka katika timu 63 za Wizara pamoja na  Idara za Serikali.

Hivyo  alisema  , ni wajibu  wa viongozi wote sehemu za kazi kuendelea kusimamia shughuli za michezo na kuhakikisha watumishi wanashiriki kikamilifu michezo ili waweze kujenga na kuwa wakakamavu wakati wa
kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Mashindano ya Shimiwi yana umuhimu wa kipekee kwetu sote , hili ni darasa tosha la vitendo katika nidhamu, mshikamano, burdani , uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja , makundi mbalimbali na Wizara kwa
ujumla” alisema Dk Mukangara. Waziri Mukangara pia aliupongeza Uongozi wa Shimiwi kwa kuamuzi wake
wakuhusisha makundi maalumu yakiwemoi ya watu wenye ulamavu katika michezo hiyo.

“ Utaratibu huu unaonesha ni kwa kiasi gani mnatambua umuhimu wa kuendeleza michezo kwa watu wenye vipaji bila kuwasahau wenzetu wenye ulemavu na mahitaji maalum …nawapongeza kwa hatua hii” alisema Waziri huyo. Hata hivyo alisema  ni matarajio yake kuwa ushiriki wa watu wenye ulemavu utaongezeka mwaka hadi mwaka na kuhusisha aina nyingi za michezo kwa lengo la kuhakikisha vipaji vya michezo vinaibuliwa na kuendelezwa kwa dhati kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine wa Serikali
bila kubaguliwa.

Waziri huo, pia aliwatahadharisha Wanamichezo hao wa Shimiwi kuwa Ukimwi bado ni tatizo kubwa hapa nchini na kasi ya maabukuzi bado ni kubwa , hivyo ni wajibu wao wasijiruhusu kujenga mazingira hatarishi
ya kuambukizana Virusi vya Ukimwi wakati wote wa michezo hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mwandishi, kweli waziri alisema hivyo ?? kwamba wanamichezo wajihadhari na maambukizi ya ukimwi katika kipindi chote cha michezo hiyo.sasa je baadaye michezo hiyo itakapomalizika ,je ? ruksa ??? mimi naona tahadhari tuifanye muda wote wa uhai wetu na ikiwezekana elimu ya kupiga kunyeto ifundishwe mashuleni. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  2. Timu ya Ikulu mko vizuri!!!!! Mnapatikana wapi baada ya mashindano haya?? nataka nije kujifunza zaidi historia ya mchezo huu wa netiboli!!! asanteni na hongereni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...