Wachezaji wa michezo ya aina mbalimbali ya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakipita mbele ya jukwaa la mgeni rasmi
Kikosi cha timu ya Ikulu, mchezo wa mpira wa netiboli , wakijpanga kabla ya kuanza mchezo
Kocha Hellen Siboka (kulia) akiwa na kikosi chake kabambe cha timu ya Ikulu kabla ya kuanza mchezo
Kikosi cha timu ya mpira wa Netiboli Ofisi ya RAS Kilimanjaro , wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukosa mshindani
![]() |
| Baadhi ya wachezaji na viongozi wa timu ya Netiboli ya Ukaguzi wakitoa uwanjani baada ya sare ya bao 27-27 dhidi ya Uchukuzi |
![]() |
| Hapa ni patashika kati ya timu ya Netiboli Wizara ya Kilimo (jezi za mchezaji aliyeshika mpira0 VS timu ya Maji leo ambapo Kilimo ilishinda bao 32- 22. |
Timu ya mpira wa Netiboli ya Ikulu, ikikaguliwa na Mwamuzi , baada ya kumaliza kuikagua timu ya Tume ya Utumishi.
Picha zote na habari John Nditi,
wa Globu ya Jamii, Morogoro
WAZIRI wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Dk Finella Mukangara, amezitaka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zihakikishe zina kuwa na bajeti ya kutosha ya michezo ili kutafsiri dhana zima ya Serilali
ya kupenda na kuhimiza michezo kazini. Pia amesema ni wajibu wa kila Wizara, Idara na Taasisi za Serikali ,Vyama vya Michezo na sehemu za jamii kuwajibika kimatendo katika kukuza na kuendeleza michezo.
Dk Mukangara alisema hayo Septemba 22, mwaka huu katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mashindano ya 32 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali ( SHIMIWI) kwa mwaka 2012 yanayofanyika Mkoani Morogoro na kuwashirikisha zaidi ya wanamichezo 3,000 kutoka katika timu 63 za Wizara pamoja na Idara za Serikali.
Hivyo alisema , ni wajibu wa viongozi wote sehemu za kazi kuendelea kusimamia shughuli za michezo na kuhakikisha watumishi wanashiriki kikamilifu michezo ili waweze kujenga na kuwa wakakamavu wakati wa
kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Mashindano ya Shimiwi yana umuhimu wa kipekee kwetu sote , hili ni darasa tosha la vitendo katika nidhamu, mshikamano, burdani , uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja , makundi mbalimbali na Wizara kwa
ujumla” alisema Dk Mukangara. Waziri Mukangara pia aliupongeza Uongozi wa Shimiwi kwa kuamuzi wake
wakuhusisha makundi maalumu yakiwemoi ya watu wenye ulamavu katika michezo hiyo.
“ Utaratibu huu unaonesha ni kwa kiasi gani mnatambua umuhimu wa kuendeleza michezo kwa watu wenye vipaji bila kuwasahau wenzetu wenye ulemavu na mahitaji maalum …nawapongeza kwa hatua hii” alisema Waziri huyo. Hata hivyo alisema ni matarajio yake kuwa ushiriki wa watu wenye ulemavu utaongezeka mwaka hadi mwaka na kuhusisha aina nyingi za michezo kwa lengo la kuhakikisha vipaji vya michezo vinaibuliwa na kuendelezwa kwa dhati kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine wa Serikali
bila kubaguliwa.
Waziri huo, pia aliwatahadharisha Wanamichezo hao wa Shimiwi kuwa Ukimwi bado ni tatizo kubwa hapa nchini na kasi ya maabukuzi bado ni kubwa , hivyo ni wajibu wao wasijiruhusu kujenga mazingira hatarishi
ya kuambukizana Virusi vya Ukimwi wakati wote wa michezo hiyo.








Mwandishi, kweli waziri alisema hivyo ?? kwamba wanamichezo wajihadhari na maambukizi ya ukimwi katika kipindi chote cha michezo hiyo.sasa je baadaye michezo hiyo itakapomalizika ,je ? ruksa ??? mimi naona tahadhari tuifanye muda wote wa uhai wetu na ikiwezekana elimu ya kupiga kunyeto ifundishwe mashuleni. Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteTimu ya Ikulu mko vizuri!!!!! Mnapatikana wapi baada ya mashindano haya?? nataka nije kujifunza zaidi historia ya mchezo huu wa netiboli!!! asanteni na hongereni sana
ReplyDelete