![]() |
Kocha wa Yanga akipokewa kwa shangwe mwezi Julai mwaka huu |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mbelgiji Tom
Saintfiet amefukuzwa kazi usiku huu, baada ya kutofautiana sera na uongozi wa
Yanga na sasa Fredy Felix Minziro, aliyekuwa Msaidizi wake, atakaimu nafasi
yake.
Habari zaidi, kuhusu
kufukuzwa kwa kocha huyo, Yanga itatoa taarifa rasmi kesho asubuhi saa 3:00,
makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Mapema leo mchana, uongozi
wa Yanga ya Dar es Salaam, ulitangaza kuisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya
klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu,
kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa
Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya
Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine wanaokumbwa na
panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa
Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kwenye majukumu
mengine.
“Tumesitisha mikataba ya
sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa timu na muda
si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti mpya,”alisema
Sanga.
Aidha, Sanga alisema Kocha
Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na vyombo vya
habari.
“Tumekwishakutana naye mara
kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa tutamuandikia
barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na
vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa ujumla maamuzi haya
yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na sare ya
bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na
Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sasa beki wa zamani wa
Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Lawrence Mwalusako atakaimu
nafasi ya Katibu wa klabu hiyo, kufuatia kusimamishwa kwa Celestine Mwesigwa,
wakati kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Sekilojo Johnson Chambua atakuwa Meneja
mpya wa klabu hiyo, akirithi mikoba ya Hafidh Saleh.
Habari kutoka ndani ya
Yanga, zimesema kwamba viongozi hao wapya watatangazwa wakati wowote kuanzia
sasa kurithi nafasi za viongozi walioondolewa madarakani, kutokana na kile
kilichoelezwa utendaji usioridhisha.
Nafasi nyingine za Mhasibu
mpya, iliyoachwa wazi na Philip Chifuka itakuwa chini ya dada mmoja, aliyetajwa
kwa jina moja tu, Rose aliyekuwa akifanya kazi ofisi hiyo kwa muda mrefu,
wakati Msemaji wa klabu iliyoachwa wazi na Louis Sendeu, inaelezwa atapewa
mdogo wa mke wa Ridhiwani Kikwete, aliyehesabu kura za Abdallah Bin Kleb katika
uchaguzi mdogo wa klabu, Julai 14.
Hizi tabia za kufukuzana tumechoka sasa..aggggh
ReplyDeleteNa mbado! Oh kikosi cha mauaji, oh kikosi cha maangamizi, kiko wapi? yeboyebooooooooooo!! hahahaaaaaaaa! Na mbado!
ReplyDeleteMTABADILI KUNI ZOTE LAKINI MOTO NI ULEULE
ReplyDeletena wewe manji unasubiri nini? ukiona mwenzio ananyolewa na wewe....shauri yako.
ReplyDeleteHuyu kocha nilimuona toka awali ni mbabaishaji ana dharau na kila mara visingizio ohh wachezaji wanasuka nywele ni kama Maximo vile maneno mengi ujuzi sifuri. Afadhali Yanga wameliona hili mapema. Yanga tafuteni kocha wa maana sasa, sio kocha maneno mengi na dharau.
ReplyDeleteJangwani hii kama ndoa ya Kim Kardashian, tuwaazime Julio kwa muda? Ha ha haaa! Na msimu huu mnyama mtamkoma kudadadeki...
ReplyDeletemambo ya mbeya hotel au? na bado, safari ijayo wachezaji watalazwa wanne kwenye kitanda cha mtu mmoja.
ReplyDeleteWewe mdau wa 1:08 PM huwezi kumlinganisha kocha wenu wa Yanga na Maximo. Maximo alipokuja nchini soka ilikuwa chini ya sifuri (minus) kwa kiwango na aliweza kuinyanyua kwa kiwango chake.
ReplyDeleteTatizo la Watanzania wanataka matokeo baada ya wiki mbili wakati timu hata kujifunza nidhamu walikuwa hawataki. Wchezaji waache bangi kwanza ndiyo waendelee na kujifunza soka.
MATATIZO SIO MAKOCHA VILABU VYETU VINA USWAHILI MWINGI SASA HATA AJE KOCHA TOKA MBINGUNI YANGA NA SIMBA ATAFUKUZWA KWA SABABU KUNA WATU WAMAJAZANA NDANI YA VILABU HIVI KAZI ZAO KUSAGA MANENO NA KUFUTA RUZUKU SASA KAMA HAWA WAPAMBE WATAENDELEA KUTAFUTA RUZUKU HUMU VILABUNI MPIRA BONGO HAMNA NA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA SPAIN AKIJA YANGA BASI WATAFUNGWA NA WATAMTAFUTIA ISSUE ILI AHAME.
ReplyDeleteNA MATAJIRI WENYEWE WA WANAOMFADHILI HUYU KOCHA HUWA WANACHACHA UPESI KWANI HUJITIA KWENYE MIKATABA YA MAPESA MENGI NA MFUKO WENYEWE UNATEGEMEA BIASHARA SASA WAKIONA KINANUKA BASI WANAFUKUZA KWA KUWA KUNA KIPENGERERE NDANI YA MKATABA KINAWARUHUSU KUFANYA HIVYO IKIWA HAWAONI MATOKEO MAZURI SASA BONGO TAJIRI AKISEMA LEO JIFUNGISHENI WACHEZAJI WANAITIKIA WITO TAJIRI ASUBUHI ANAMSHIKIA KIUNO KOCHA KUWA HAFAI BORA ARUDI NYUMBANI HAYO YAMETOKEA HUKO NYUMA SASA MPIRA NAONA UNATUSHINDA TUJARIBU TARABU HUENDA TUKAWAPITA ZENJ.
tatizo sio makocha domo jingi humu vilabuni utafikiri vilabu vya pombe.
ReplyDeletemdau.
bangladesh.
Eti nasikia alikuwa SHOGA! Ni kweli?
ReplyDeleteMbelgiji akaandae maziwa ya mtindi kiwandani kwao huko.
ReplyDelete