Kocha wa Yanga akipokewa kwa shangwe mwezi Julai mwaka huu

Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mbelgiji Tom Saintfiet amefukuzwa kazi usiku huu, baada ya kutofautiana sera na uongozi wa Yanga na sasa Fredy Felix Minziro, aliyekuwa Msaidizi wake, atakaimu nafasi yake.
Habari zaidi, kuhusu kufukuzwa kwa kocha huyo, Yanga itatoa taarifa rasmi kesho asubuhi saa 3:00, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Mapema leo mchana, uongozi wa Yanga ya Dar es Salaam, ulitangaza kuisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine wanaokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kwenye majukumu mengine.
“Tumesitisha mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti mpya,”alisema Sanga. 
Aidha, Sanga alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa tutamuandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa ujumla maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sasa beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Lawrence Mwalusako atakaimu nafasi ya Katibu wa klabu hiyo, kufuatia kusimamishwa kwa Celestine Mwesigwa, wakati kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Sekilojo Johnson Chambua atakuwa Meneja mpya wa klabu hiyo, akirithi mikoba ya Hafidh Saleh.
Habari kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba viongozi hao wapya watatangazwa wakati wowote kuanzia sasa kurithi nafasi za viongozi walioondolewa madarakani, kutokana na kile kilichoelezwa utendaji usioridhisha.
Nafasi nyingine za Mhasibu mpya, iliyoachwa wazi na Philip Chifuka itakuwa chini ya dada mmoja, aliyetajwa kwa jina moja tu, Rose aliyekuwa akifanya kazi ofisi hiyo kwa muda mrefu, wakati Msemaji wa klabu iliyoachwa wazi na Louis Sendeu, inaelezwa atapewa mdogo wa mke wa Ridhiwani Kikwete, aliyehesabu kura za Abdallah Bin Kleb katika uchaguzi mdogo wa klabu, Julai 14.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hizi tabia za kufukuzana tumechoka sasa..aggggh

    ReplyDelete
  2. Na mbado! Oh kikosi cha mauaji, oh kikosi cha maangamizi, kiko wapi? yeboyebooooooooooo!! hahahaaaaaaaa! Na mbado!

    ReplyDelete
  3. MTABADILI KUNI ZOTE LAKINI MOTO NI ULEULE

    ReplyDelete
  4. na wewe manji unasubiri nini? ukiona mwenzio ananyolewa na wewe....shauri yako.

    ReplyDelete
  5. Huyu kocha nilimuona toka awali ni mbabaishaji ana dharau na kila mara visingizio ohh wachezaji wanasuka nywele ni kama Maximo vile maneno mengi ujuzi sifuri. Afadhali Yanga wameliona hili mapema. Yanga tafuteni kocha wa maana sasa, sio kocha maneno mengi na dharau.

    ReplyDelete
  6. Jangwani hii kama ndoa ya Kim Kardashian, tuwaazime Julio kwa muda? Ha ha haaa! Na msimu huu mnyama mtamkoma kudadadeki...

    ReplyDelete
  7. mambo ya mbeya hotel au? na bado, safari ijayo wachezaji watalazwa wanne kwenye kitanda cha mtu mmoja.

    ReplyDelete
  8. Wewe mdau wa 1:08 PM huwezi kumlinganisha kocha wenu wa Yanga na Maximo. Maximo alipokuja nchini soka ilikuwa chini ya sifuri (minus) kwa kiwango na aliweza kuinyanyua kwa kiwango chake.

    Tatizo la Watanzania wanataka matokeo baada ya wiki mbili wakati timu hata kujifunza nidhamu walikuwa hawataki. Wchezaji waache bangi kwanza ndiyo waendelee na kujifunza soka.

    ReplyDelete
  9. MATATIZO SIO MAKOCHA VILABU VYETU VINA USWAHILI MWINGI SASA HATA AJE KOCHA TOKA MBINGUNI YANGA NA SIMBA ATAFUKUZWA KWA SABABU KUNA WATU WAMAJAZANA NDANI YA VILABU HIVI KAZI ZAO KUSAGA MANENO NA KUFUTA RUZUKU SASA KAMA HAWA WAPAMBE WATAENDELEA KUTAFUTA RUZUKU HUMU VILABUNI MPIRA BONGO HAMNA NA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA SPAIN AKIJA YANGA BASI WATAFUNGWA NA WATAMTAFUTIA ISSUE ILI AHAME.
    NA MATAJIRI WENYEWE WA WANAOMFADHILI HUYU KOCHA HUWA WANACHACHA UPESI KWANI HUJITIA KWENYE MIKATABA YA MAPESA MENGI NA MFUKO WENYEWE UNATEGEMEA BIASHARA SASA WAKIONA KINANUKA BASI WANAFUKUZA KWA KUWA KUNA KIPENGERERE NDANI YA MKATABA KINAWARUHUSU KUFANYA HIVYO IKIWA HAWAONI MATOKEO MAZURI SASA BONGO TAJIRI AKISEMA LEO JIFUNGISHENI WACHEZAJI WANAITIKIA WITO TAJIRI ASUBUHI ANAMSHIKIA KIUNO KOCHA KUWA HAFAI BORA ARUDI NYUMBANI HAYO YAMETOKEA HUKO NYUMA SASA MPIRA NAONA UNATUSHINDA TUJARIBU TARABU HUENDA TUKAWAPITA ZENJ.

    ReplyDelete
  10. tatizo sio makocha domo jingi humu vilabuni utafikiri vilabu vya pombe.
    mdau.
    bangladesh.

    ReplyDelete
  11. Eti nasikia alikuwa SHOGA! Ni kweli?

    ReplyDelete
  12. Mbelgiji akaandae maziwa ya mtindi kiwandani kwao huko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...