Msafara maarufu duniani unaojulikana kama 'Annual animal Migration' unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu umeanza kurejea katika makazi yao ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakitokea mapumziko ya mwezi mmoja katika nchi ya jirani ya Kenya, hususan  kwenye mbuya ya Masai Mara.

Kila mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala hufanya mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi kati ya hiyo huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na iliyobaki hutumiwa na wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
Mwaka huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na ambao hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana kurejea nchini ukitokea mapumziko.
 Kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu hali hii inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti ambapo imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa wanayama hawa.
Changamoto kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio la kuvuka Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko ambao nao huwa ni msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye kuwakamata wanyama hawa mara wanapovuka mto.
Watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakifurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la kuvuka Mto Mara ambalo wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali zilizotengenezwa katika eneo hili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. MICHUZI HUMECHEMSHA MAMBA SIO MNYAMA NI REPTILE HUTAGA MAYAI NA.. HAPO REKEBISHA

    ReplyDelete
  2. Anony Mon Sep 17, 02:58:00 AM 2012>>>>>>Unadai Mamba sio mnyama anataga mayai Haya Tuambie wewe mamba ni ndege au kitu kani, au tueleze REPTILE kwa kiswahili maana yake nini.

    ReplyDelete
  3. Michuzi yuko sahihi kwa kuwa mamba ni wanyama. Kitaalam himaya ya wanyama "kingdom animalia" hujumuisha Raptilia, amphibia, Ndege,samaki na mammalia

    ReplyDelete
  4. Kumbe Utalii kwa kila kiumbe ?

    Sisi tunatalii kwenda kuwatazama wanyama huko Serengeti na Manyara na wao wanapata muda fulani wanakwenda matembezi Kenya na sasa ndio wanashuhudiwa na sisi tukiwapokea wakirudi!

    Ndio maana Haki inazingatiwa pia kwa viumbe kama wanyama!

    ReplyDelete
  5. duh wanyama huenda vacation, sie binadamu tumetingwa we cannot afford one......tafakari kisha chukua hatua

    ReplyDelete
  6. anony sasa tuambie basi reptile ni nini kwa kiswahili tuelewe.

    ReplyDelete
  7. ANONY WA KWANZA HAPO JUU, HATA WEWE UMECHEMSHA. HAKUNA NENO LA KISWAHILI "HUMECHEMSHA" BALI NENO SAHIHI NI "UMECHEMSHA"... HAPO JIREKEBISHE.

    ReplyDelete
  8. Ankali kwa kauli yako hapa utawatonesha kidonda Watani wetu wa Jadi Kenya !

    ''....msafara wa nyumbu ukitokea mapumziko ya mwezi mmoja huko nchini Kenya! ''

    Ina maana kwa kauli hiyo nyumbu makazi yao na kwao ni Tanzania?

    ReplyDelete
  9. Wakenya tumewazoea na Publicity yao, eti Mlima kilimanjaro upo Kenya. Nilim umbua Mkenya Mmoja hapa ugaibuni akidanganya. Sema sio Siri Tanzania haifahamiki sasa sijui Wizara ya Mali asili chini ya Tanzania Tourists Board wanafanya nini. Kazi kusafiri tu na kujiongezea Madokezo kazi hawaifanyi ipasavyo.

    ReplyDelete
  10. naunga mkono anony wa apo juu kweli Tz aijulikani hata kidogo yani nipo ugaibuni naulinzwa unatokea nchi gani nikitaja Tanzania wananishangaa kwanza iko wapi? ukitaja kenya fasta wanakuelewa eti huyu waziri anayehusika na wizara nyeti kama hii anafanya niniiii?kizazi cha sasa hakifahamu Tanzania wazeee ndo wanafahamu kwa sababu ya nyerere,Tanzania Amkaaaaa

    ReplyDelete

  11. Anon wa Sep 17 03:12:00 PM na Sep 18 04:41:00 AM

    Wengi wa watu wa huko ughaibuni wako na 'closed minds' when it comes to geography, sio kama sisi huku tunaofundishwa geography ya dunia. Umbumbumbu wao kwenye geografia pia unachangia, nani asieijua Zanzibar iko wapi na Kilimanjaro iko wapi leo hii?

    Na wewe unaesema 'HUMECHEMSHA' wadau wamekupa darasa, generally mamba ni mnyama.
    Mdau wa Sep 17 10:05:00 AM endelea kusomesha, PAPA PIA ANAITWA ANIMAL.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...