Bandari Tanga wakiingia uwanjani kabla ya kuanza kwa michezo.

Michezo ya Bandari maarufu kama ‘inter-ports games’ imeanza rasmi katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mashabiki wameonesha kuridhishwa na michezo ya awali ya ufunguzi huku wachezaji wakionesha vipaji vya hali ya juu katika michezo ya soka, mpira wa kikapu, pete na kuvuta kamba. 

Michezo hiyo ambayo imefunguliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (MB), aliyefurahishwa na kuridhishwa na maandalizi yake, inategemewa kufanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Agosti 15 katika jiji la Mwanza. Dk. Tizeba amewaasa wachezaji kucheza kwa upendo na staha na kukumbuka kwamba michezo inajenga undugu na mshikamano na si uadui. 

Aidha amewakumbusha wachezaji kuendelea kushiriki katika michezo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha afya zao mara baada ya kukamilka kwa michezo hii. 

Michezo ya ‘inter-ports games’ inazikutanisha bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu ambapo michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba, bao, riadha, kikapu na mprira wa pete itashindaniwa.
Mpira wa pete ulikuwa ni kivutio cha aina yake. 

kwa picha zaidi
bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...