Sijui kama unakumbuka kwamba miaka kadhaa tu iliyopita,muziki wa mwambao au taarabu au mipasho ulikuwa “juu’ kushinda ambavyo ungedhania. Kisha,kama yalivyo mambo mengine mengi,ile hali ikapita. 

Bongo Hip Hop ikateka.Kisha Bongo Fleva ikawa mfalme wa mitaa.
Miaka kadhaa baadae,watu wa mwambao au taarab wakaibuka upya.Ndipo majina kama Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na wengineo wakatukumbusha kwamba hii miziki mingine, bado tunakandamizia sana kama anavyoasa Muhogo Mchungu. 

Pengine kilichokuwa kinakosekana ni ule utambuzi kwamba, ushirikiano katika sanaa ni jambo jema kama ambavyo ni jema kwa wanasiasa ingawa kundi hilo limekuwa gumu zaidi katika kushirikiana.
Katika kuonyesha kwamba ushirikiano ni mzuri na unaweza kutoa kitu kizuri, Producer Lamar anacho kitu. Ni ushirikiano wa Isha Mashauzi na Banana Zorro katika wimbo "Ukinipenda". 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nice 'duet' nyimbo imetulia na nzuri, kuanzia mziki wake mpaka ujumbe iliyobeba . Nawapongeza sana Isha Mashauzi & Banana Zorro.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...