Rais Yoweri Museveni wa Uganda akimkaribisha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye sherehe za maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala,Uganda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gaharib Bilal (kulia) akibadilishana mawazo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda. Sherehe hizo zimefanyika jana katika Uwanja wa Kololo jijini Kampala. Wanaoonekana nyuma yao ni wake zao, Bibi Janneth Museveni (kulia) na Mama Zakia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda kwenye Uwanja wa Kololo, jijini Kampala jana. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Somalia Hassan Shekhe Mahamoud na Makamu Rais wa Sudan, Bwana Haji Adam Yusufu.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akihudhuria Mkutano wa tano wa Viongozi Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyia kwenye Ukumbi wa Commonwealth wa Hotel ya Munyonyo jijini Kamapala jana. Wengine kutoka kushoto ni Rais Paul Kagame wa Rwanda na Makamu wa Rais wa Sudan, Haji Adamu Yusufu.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...