Mgambo wa Jiji la Dar es Salaam mchana wa leo wameendesha zoezi lao la kuwaondoa wafanya biashara ndogo ndogo (maarufu kama wamachinga) maeneo ya katikati ya jiji,hali hii imeleta  malalamiko mengi kutoka kwa wafanya biashara hao, ambao wamilalamikia kwamba wanaonewa,kwani wao wameamua kujitafutia riziki kihalali katika maeneo yasiyo rasmi kwa mujibu wa halmashauri ya jiji la Dar. Ila Wafanya Biashara hao wamelalamikia utaratibu unaotumiwa na Mgambo hao wa kukamata biashara zao na kwenda nazo wanakokujua wao.
Mgambo wa Jiji wakipakia kwenye Gari vifaa mbali mbali vinavyotumiwa na Wamachinga hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. TUMUOGOPENI MUNGU JAMANI....mtu maskini kama huyu anatafuta riski yake akale na watoto wake bila ya kumuibia mtu, leo unakwenda kumtupia biashara yake kweli jamani hii inaingia akilini,

    kesho anaamka huyu mtu hajui aanzie wapi na watoto wake maskini ya mungu kwanini musiwape kibali ikawa wao ni mobile ...

    jifikirieni kama ingekuwa hii hali unayo wewe na umaskini huu wa nchi hii na jua hili wapi wengeelekea , huku ukiambiwa mtoto anahitajia kwenda shule na mwengine yuko na malaria anahitajia umpeleke hospital na mote humo munahitajia pesa wakati wewe hapa pesa ya kula hunayo tena

    jamani maisha ni magumu sana hapa dar au tanzania kwa ujumla sasa leo hii unafanya ushenzi kama huu kumwaga chakula cha mtu, na je mtu huyu huyu akija usiku akikuibia wewe ndani utapiga kelele ila jua kuwa ni wewe ndio uliemsababishia yote haya

    katika hali kama hii tufikiriane sana mwenye nacho ajuwe kuwa kuna mtu mwengine hata mlo mmoja wa leo hii haujui ataupata vipi, na hii sio huyu tu wako wengi au tuko wengi sana tushapitia hali halisi ya maisha na ugumu wake naujuwa mimi kwani nishapitia kwenye dhiki na najuwa machungu yake, sasa basi kwa nyinyi wenzangu ambao bado hamjapita kwenye maisha ya shida wafikirieni sana walo na shida ambao ndio waliowengi sana tanzania hii,

    shukran sana haya ni mawazo yangu tu,

    ReplyDelete
  2. nchi hiyo roho mbaya kuanzia watumishi wa juu wa serikali mpaka watumishi wadogo hakuna mwenye roho ya imani

    sasa hao wanaojitafutia kwa njia halali mnawatesa namna hiyo?

    na hizo bidhaa zao mnazitupa ndani ya malori hivi watazipata wenyewe kweli?

    masikini wengine wamekopa msingi leo hii mnawafanyia hivyo

    haki ya nani tena nchi hiyo ni mbovu sana yani nchi ya kinyama.

    mdau wa Peru

    ReplyDelete
  3. Tanzania yenu hiyo kama new york.

    ReplyDelete
  4. poleni sana malofa wenzangu ( machingaz) INSHAALLAH Mungu yupo na anaona kila kitu, jasho la mnyonge halipotei......HUU NI UOEVU ULIO WAZI MASKINI, HAWA WATU WAKALE WAPI? KILA WANACHOKIFANYA KWAO NI KOSA, WENGINE MITAJI YAO WAMEKOPA . EWE MOLA MUUMBA MINGU NA ARDHI, WASAIDIE WANYONGE WAKO WANAONEWA, HAWANA MTETEZI, VIONGOZI KARIBIA WOOOTE WANAFKI WANAJALI MATUMBO YAO.

    ReplyDelete
  5. Kuwaondoa watu wakitafuta riziki yao bila ya kuwatafutia kazi nyingine ni uonevu wa haki ya binadamu. Watanzania ni wapole sana, jaribu kufanya hivyo nchi kama India au Indonesia, utaona wananchi wataandamana na kutupa mawe mpaka serikali utakoma. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Mfanyakazi masikini anafanya kazi kwa bidii bila ya kuiba, nyinyi mtachukua riziki yake. Iku siku mtajuta. Na siku hio ipo karibu sana.

    ReplyDelete
  6. bwana eh, kama unataka kufanya mobile business basi kuna njia sahihi za kufanya - ni swala la kujiorodhesha kihalali, ulipe kodi stahiki uendelee kufanya biashara raha mustarehe. Tatizo machinga wengi hawataki hilo la kujisajili wawe legit business.

    Isitoshe, machinga complex imejengwa kwa ajili yao - waende wakaitumie basi.

    Nchi zilizoendelea e.g. USA, hakuna machinga mtaani ila kuna eneo kubwa sana maeneo mbalimbali ambapo wafanyabiashara wanaenda kuuza vitu vyao bila ya kubughudhiwa, wanaziita "flea markets". Ukitaka vitu wanavyouza machinga mtaani mteja unakwenda huko kwa muda wako. Ukiwa unauza chakula mjini basi unapata leseni ya kufanya hivyo inayozingatia usafi, sheria, vibali etc.

    Its about time Tanzania tuanze kuangalia kufanya mambo kama haya.

    ReplyDelete
  7. WE ANONY HAPO, ACHA KUTUONGOPEA.. LOH!

    Nawasiwasi kama unalipa kodi kweli!!! Sisi wenyewe tunaolipa kodi pesa nyingi sana kila mwezi na bado hatuoni kodi yetu inafanya kitu gani, zaidi ya kuona pesa hizo zikiishia mikononi mwa watu wachache na wakwepa ushuru bandarini kibao.

    Hizo biashara ndogo sana kwenye kodi ni sawa na tone la maji, baharini. Watafutieni maeneo safi ya kufanya biashara na wananchi tutawafuata huko, tuone kama wataonekana barabarani.

    ReplyDelete
  8. Wajameni, hizi kwanini mko busy na kutafuta ULAJI, RUSHWA N.K. KWA MACHINGA, tuomba hayo malori yatumike kuzoa takataka na michanga barabara za M/nyamala, Makumbusho, Kijitonyama, Mikocheni na Sinza na vitongoji vyao. Siyo kufagia kwa kusogeza pembeni kisha mvua ikija mchanga unarudi tena barabarani. EBO! uzolewe.

    Sijaona KABISA juhudi za makusudi za viongozi wetu ukianzia na Mkuu wa Mkoa wa DSM, na safu yako yote ya uongozi, vipi JIJI limewansinda?!!!

    ReplyDelete
  9. Huo si uonevu, wananchi wanatakiwa watii sheria. Kuwa na biashara si tiketi ya kuvunja sheria, hata kama ni biashara fanya zile sehemu zinazohusika...nenda sokoni siyo kila mahali kusumbua wasiotaka kununua. Kwanini wasiende sokoni? Kariokoo? kwingineko? wanajazana katikati ya miji yetu kuleta bughudha na makelele. Hatukatai kufanya biashara lakini kuwe na utaratibu maalumu...kwani mbona biashara nyingi tu zina utaratibu na zinafanyika vizuri tu. Mteja akihitaji mwavuli au chochote kile atafunga safari kufuata, TUMECHOKA KUBUGHUDHIWA NA MACHINGA, FUJO NA WIZI ZIMETUCHOSHA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...