Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu cha Masai Football Club ya Mto ya Makuyuni,Monduli mkoani Arusha kikiwa katika picha ya pamoja.Timu hii imetoa majigambo ya kwamba hakuna timu yeyote itakayoweza kuchukua point mikononi mwao kwani wao wako fiti kikweli kweli.
 Mtanange wa kujipima nguvu kwa timu hiyo ukiendelea katika uwanja wa Chuo cha Ualimu,Monduli.
 Mchezaji wa timu hiyo akiendelea kuchanja mbuga wakati wa mchezo wa kujipima nguvu.
 Hapa hapiti mtu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. ilikua majira ya mchana ama usiku?

    ReplyDelete
  2. Hukusikia vizuri, sikusema kwamba hawajui kucheza mpira, nilisema; hawachezagi mpira mchana.

    ReplyDelete
  3. Unajua hawa wenzetu wanachosema ni kweli...hakuna atakayewaweza kama mazingira ya kuchezea ndo haya...wanachezea gizani, wana night vision eyes kama simba. Wewe ukicheza nao mpira utauona wapi? Mdau,CA-USA

    ReplyDelete
  4. Duh! we mdau kiboko..unasema "hukusikia vizuri..... hapo umendiaka au umesem? nilidhani ungesema hukusoma vizuri!!!

    ReplyDelete
  5. ......halafu wnacheza na sime zao viunoni, ukimlamba chenga anachomoa sime!!

    ReplyDelete
  6. Sisi Maasai wooote ni Yanga S.C sababu ni nini?

    Simba ni adui yetu nakula ng'ombe setu kwa Boma!

    ReplyDelete
  7. du kwa mtaji huo wakucheza na panga lazima ufungwe!!1

    ReplyDelete
  8. ukimpiga chenga mbaya, anatoa jambia, lazima utamwachia mpira!

    ReplyDelete
  9. Chonde chonde jamani sime hizooo.......

    ReplyDelete
  10. Kiboko ni pale watakapopiga msamba, silaha za maangamizi zaidi zitaanikwa hivyo wakwe msiende uwanjani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...