Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakiwa wameketi kwenye madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 waliyokabidhiwa na Benki ya NMB kama sehemu ya msaada kwa shule hiyo.
Meneja wa NMB Bank House Bw. Leon Ngowi (kulia) akimkabidhi dawati moja kati ya madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotolewa na NMB Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge Bi. Hadija Telela. Wakishuhudia ni Meneja Huduma kwa Wateja wa NMB Bank House, Stephen Chavalla (Pili kushoto) na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Bunge Christina Wambura.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge iliyopo katika Manispaa ya Ilala, wakifurahia madawati 50 yaliyotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa madawati shuleni hapo.





naona mashirika tu ndio yanayosaidia misaada ya mashuleni
ReplyDeleteje zile hela za rada zilizolipwa tukaambiwa zitatumika kwajili ya vifaa vya mashuleni zimeenda wapi wajemeni mwe! inji hii mbona kazi